Caf ya sasa hivi rahisi kuliko ya zamani.. zamani kufika group stage tu ilikuwa uwe mwanaume kweli kweli.... maana group stage zilikuwa zinaingia timu 8 tu.. siku hizi group stage zinaingia timu 16..
Enyimba waliwekeza hela nyingii sana kutwaa ubingwa wa caf haraka haraka. Walijenga hadi uwanja wa gharama kuliko hata wa mazembe ama azam... enzi hizo waarabu kina zamalek, al ahly, esperence, es setif, waydad, raja casablanca walikuwa wa moto kweli kweli, huku kwa weusi kuna asec mimosas, mazembe,canon yaunde, asante kotoko etc, hapo jiulize makundi tu unafikaje katika nafasi 8 tu, na hapo hapo ukatwae ubingwa kabisa
Zama hizi hakuna wachezaji wa kiwango kama zamani kwa timu za africa zinazocheza caf maana ulaya wanaenda mapema , mfano aboutrika, zaki, enyeama, toure, etc etc walikuwa wana uwezo mkubwa sana na wanacheza caf na timu zao huku wana viwango vya ulaya tupu
Caf wamefanya mabadiliko mengi kwenye mashindano yao yote. Yamekuwa mepesi ndio maana hata Tanzania tunafuzu kucheza afcon zama hizi.... zamani wewe ulisikia wapi nchi kama Tanzania ama kenya na burundi zinafuzu afcon.
Kwanza hata kwa zama hizi horoya ana mafanikio ya haraka kuliko simba .. na horoya hawajawekeza hela nyingi kama simba .ila horoya anafika mbali kuliko simba karibu kila msimu