Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa ruhusa kwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kutumika kwa michezo ya robo fainali na nusu fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) kwa msimu wa 2024/2025.
Ruhusa hii imekuja baada ya ukaguzi wa kina uliofanywa na wakaguzi wa CAF hivi karibuni, ambapo uwanja huo umeonekana kuzingatia viwango vya kimataifa vya michezo. Hata hivyo, CAF itaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea kwenye uwanja huo kuhakikisha unakidhi matakwa ya michuano hiyo mikubwa.