Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam umeondolewa katika orodha ya viwanja vilivyoidhinishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutokana na kuendelea kwa matengenezo makubwa yanayoandaliwa kuelekea AFCON 2027.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa uwanja huo hautatumika kwa muda katika mashindano ya CAF hadi pale matengenezo yatakapokamilika.
Wakati huo huo, Uwanja wa Azam uliopo Chamazi umepewa idhini ya muda tu na CAF kwa ajili ya hatua za awali za mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2026/27.