CAF yaamua mechi zote mbili za Namungo FC Vs. CD1 Agosto ya Angola kuchezwa Tanzania

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika ( CAF) baada ya kujiridhisha kuwa timu zote mbili hazikuhusika kukwamisha mchezo uliopangwa kufanyika Februari 14 nchini Angola.

Kamati ya CAF imeagiza kuwa mechi zote mbili ziwe zimechezwa kufikia Februari 26, 2021.

Timu ya Agosto kutoka Angola ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza itawajibika kulipia gharama za maandalizi ikiwemo maofisa wa mechi hiyo.

TFF
 
Uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Soka Afrika ( CAF) baada ya kujiridhisha kuwa timu zote mbili hazikuhusika kukwamisha mchezo wa awali

Mechi zote mbili ziwe zimechezwa kabla ya Februari 26, 2021 huku Agosto ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza.
Sasa Namungo washindwe wenyewe kimbinu na kisaikolojia! (home advantage).
 
CAF sijui wametumia vigezo gani Japo ni habari njema
CAF Wamesema uchunguzi wao wamebaini kuwa si Agosto wala Namungo waliohusika moja kwa moja kukwamisha kutopigwa mechi ya February 14 nchini Angola
 
CAF Wamesema uchunguzi wao wamebaini kuwa si Agosto wala Namungo waliohusika moja kwa moja kukwamisha kutopigwa mechi ya February 14 nchini Angola
Nyuma ya pazia agosto alihusika tu sasa CAF hawawezi kuwafungia na kuharibu ratiba nzima kilivhofanyika ni kuwaadhibu waangola kisayansi. Kama huanini hili halitajitokeza tena kwa wana angola kufanya walicho kifanya
 
Serikali yao haitawaruhusu de agosto kuja Bongo kucheza dhidi ya wachezaji walewale waliowatuhumu kuwa wote wanakorona na kutaka kuwaweka karantini kwa siku 14.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…