CAF yaamua mechi zote mbili za Namungo FC Vs. CD1 Agosto ya Angola kuchezwa Tanzania

CAF yaamua mechi zote mbili za Namungo FC Vs. CD1 Agosto ya Angola kuchezwa Tanzania

Hapo nimeelewa
Yes. Kwasababu hata wakisema mechi ipigwe Uganda kwa vile wote hawana makosa, hapo Namungo anakuwa hatendewi haki kutokana na gharama za safari, kwamaana anatalazimika kusafiri mara mbili wakati Agosto mara moja.

Ndo wakaamua game ipigwe huko TANZANIA ili Agosto awe amesafiri kufika Tz kama ambavyo Namungo alivyofika Angola
 
Hii kama tungefanyiwa sisi ingekua balaa moto wake.
 
Mhimu kukaza tu unaweza ukawa na mashabiki wa kutosha nyumbani kwako na kipondo kikakuhusu Kama ilivyo kuwa kwa vita congo.
 
Uamuzi huo umefikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika ( CAF) baada ya kujiridhisha kuwa timu zote mbili hazikuhusika kukwamisha mchezo uliopangwa kufanyika Februari 14 nchinii Angola.

Kamati ya CAF imeagiza kuwa mechi zote mbili ziwe zimechezwa kufikia Februari 26, 2021.


Timu ya Agosto ya Angola ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza itawajibika kulipia gharama za maandalizi ikiwemo maofisa wa mechi hiyo

TFF
Safi sana
 
watabaki mdomo wazi pale watapoona wale wachezaji wa namungo waliothibitishwa kua wana corona nao wanakipiga siku hiyo
Si wako karantini,kutoka kule lazima wawe wamepona so hata wakicheza hapakuwepo wasiwasi
 
CAF wameona aibu kuwapa Namungo ushindi wa mezani, sababu waliyoitoa kufuta mechi ya kwanza haieleweki, kama hao Agosto hawakuhusika sasa kwanini hiyo mechi isichezwe Angola? ni kina nani waliohusika? wameona wawalainishie Namungo kiaina, sasa hapo Namungo wakishindwa kwenda makundi wamelogwa.
 
Mhimu kukaza tu unaweza ukawa na mashabiki wa kutosha nyumbani kwako na kipondo kikakuhusu Kama ilivyo kuwa kwa vita congo.
Tena mara mbili zote unakula nyundo. Mpira sio kitu cha mzaaa. Barca jana kala nne nyumbani
 
Hakuna match hapo, hao waangola uwezekano wa kuto kuja ni mkubwa sana.

Halafu baada ya match wakishinda tuu, tunawapima na wote wanakuwa na corona.. tutawaweke lugalo jeshini wiki 2 hadi wapate akili
Ili nanyie mfutiwe mechi tena
 
Ni fursa adimu kwa timu ya Namongo kutumia bahati hii kuweza kusonga mbele.Yajayo kwa timu yetu ya Tanzania yanafurahisha.Ole wenu mtuangushe sisi watanzania
 
Back
Top Bottom