Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
CAF (Confederetaion of African Football) yathibitisha mabadiliko kwenye muda na uongezwaji wa washiriki kwenye michuano ya Africa Cup of Nations (AFCON) kuanzia 2019 kufuatia kongamano la kwanza la CAF nchini Morocco.
Wadau kutoka sehemu tofauti tofauti kwenye bara zima la Africa walialikwa kwa ajili ya makusudio mbalimbali yanayohusiana na maswala ya mpira wa miguu wa Africa kwenye kongamano hilo. Jana usiku CAF imetoa tamko kuthibitisha mabadiliko katika michuano ya AFCON kuwa miongoni kwa ajenda hizo.
Inatarajiwa, kuanzia 2019 na kuendelea, michuano ya Africa Cup of Nations itakuwa ikichezwa mwezi wa sita (June) na wa saba(July), na pia itahusisha timu 24 ikiwa ni timu nane zaidi ya zinazoshiriki kwenye mfumo wa sasa.
Pia CAF imesema mishuano hiyo itaendelea kuchezwa kila baada ya miaka miwili na itachezwa kwenye bara la Africa pekee.