CAF yaifutia uanachama Zanzibar yasema haiwezi kuwa na vyama viwili kutoka Tanzania

CAF yaifutia uanachama Zanzibar yasema haiwezi kuwa na vyama viwili kutoka Tanzania

Kwa hiyo Yanga (bingwa bara) na Simba (bingwa FA) itabidi wacheze na wenzao wa Zenji ili tupate wawakilishi halali wa TZ kwenye klabu bingwa Africa na shirikisho kwa msimu huu.
 
Sasa mbona wanacheza kilabu bingwa afrika na pia wanacheza shirikisho kwa kilabu zao kuwakilisha
 
Inasemekana shirikisho la mpira Africa limeiondolea uanachama Zanzibar ikiwa ni miezi michache tu ilipopewa uanachama.
Sababu iliyotolewa ni kwamba Zanzibar ni Tanzania hivyo haiwezi kuruhusu nchi moja kuwa na timu 2.
SOURCE TBC1 & BBC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walipewa uanachama bila kupitia vizuri kanuni ambazo ziko wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na sheria zingepitiwa kiufasaha wasingepewa uanachama”

Sababu kubwa ambayo CAF wameivua uanachama Zanzibar ni kutokana na kisiwa hicho kuwa ndani ya Tanzania ambao nao ni wanachama wa CAF.

Jina la nchi linatokana na jina linaloandikwa katika umoja wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo inafahamika ipo ndani ya nchi iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa CAF.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina maana lazima TFF itengeneze taratibu za kuwapata wawakilishi katika mashindano ya CAF mwaka huu au wataendelea walewale waliopatikana awali?
 
Badala ya wachangiaji kutoa madukuduku yao ya kisiasa na ya kibinafsi, ni vyema kujiuliza iwapo hii ni mara ya kwanza kwa Rais mpya wa CAF kujua juu ya uanachama wa Zanzibar, tujiulize iwapo kulikuwa kuna upinzani wowote kwenye Kikao cha CAF kilichoipa Zanzibar uanachama, tujiulize iwapo uanachama wa Zanzibar ndani ya CAF ilikuwa ni ajenda mojawapo ya Kikao cha Morocco, tujiulize iwapo Tanzania yenyewe imeilalamikia CAF juu ya Zanzibar kupewa uanachama wa CAF. Ikiwa jawabu ya yote hayo ni hapana (na ndivyo ilivyo) tujiulize basi kulikoni? Natamani tungekuwa na waandishi mahiri wa makala za uchunguzi, wakaanza kazi huku Zanzibar kujua kinachoendelea baada ya Zanzibar kupewa uanachama wa CAF. Kumekuwa na kuwindana baina ya viongozi wa ZFA kiasi cha wengine kufungiwa maisha kijishughulisha na maswala ya soka, kumekuwa na ukaidi wa kurekebisha Katiba ya ZFA ili iendane na matakwa ya CAF, kumekuwa na Utawala usioridhisha wa fedha zinazotoka CAF kiasi cha viongozi kutofautiana, kumekuwa na siasa kwenye ushiriki wa Ligi Kuu ya huku unaolazimisha kila kisiwa (baina ya Unguja na Pemba) kuwe na uwakilishi wa timu, imefikia uamuzi wa kupunguza timu kutoka 40 za mfumo huo wa kisiasa hadi 12 mwafaka na Ligi za CAF umefikiwa kwa kupiga kura, sita kwa kila kisiwa............ Timu kadhaa zilizoathiriwa na maamuzi hayo na kujikuta zikishuka daraja kabla hata ya msimu kuanza hazikuridhika na hilo. Nina taarifa za uhakika kwamba angalau mbili kati ya hizo zimepeleka malalamiko yao CAF.
Sasa kwa kuzingatia hayo, na kwa CAF kubaini kwamba imedanganywa na ZFA (kwa kuwatumia Katiba nzuri ilhali siyo wanayoitumia), na kwa kuzingatia kwamba tangu awali uanachama wa Zanzibar ulikuwa ni hisani zaidi kuliko haki yao, mtu angetegemea CAF ifanye nini kama si kukata mzizi wa fitina? Na baada ya kufanya hivyo mtu ungetegemea CAF itoe sababu zote hizo zitazoonesha udhaifu wake yenyewe ilhali sababu rahisi na ya msingi ipo? Wa kulaumiwa kwa hili ni ZFA yenyewe, na Serikali ya Zanzibar kwa kukubali kudanganywa na ZFA na kwa hivyo isichukue hatua stahiki za kuondoa kasoro zote hizo. Hapo kusingekuwa na swala la Serikali kuingilia soka, bali la Serikali kuitaka soka iendeshwe ki-FIFA na ki-CAF.
 
Walikurupuka Mkuu.

Wakati wanawapa uanachama waliambiwa kuwa Zanzibar ni nchi au sehemu ya Tanzania? Walitumia vigezo vipi kukubali maombi ya ZFA?

Ubabaishaji everywhere
 
Shirikisho la Soka Barani Afrika(CAF) leo limeifutia uanachama wa Zanzibar ikiwa ni miezi 4 baada ya kupewa uanachama huo.

Rais wa CAF amesema kuwa wamechukua uamuzi huo kwakuwa hawawezi kuruhusu kuwa na vyama viwili kutoka nchi moja(Yaani TFF na ZFA).
Hivi CAF haifahamu kwamba Zanzibar ni nchi ?
 
Back
Top Bottom