CAF yaipanga Yanga kumenyana na Sagrada Esperanca kombe la shirikisho

CAF yaipanga Yanga kumenyana na Sagrada Esperanca kombe la shirikisho

0,3470f359-cafe-425b-aa24-73d93b58f8e7.jpg

Hao hapo wapinzani wa Yanga.
 
DROO YA KOMBE LA SHIRIKISHO IMEFANYIKA MUDA SI MREFU NA WAWAKILISHI WA TANZANIA YANGA YA DAR ES SALAAM IMEPANGWA KUWAVAA WAANGOLA
========================================================
Baada ya klabu ya Dar es Salaam Young Africans kuondolewa katika michuano ya klabu Bingwa barani Afrika usiku wa April 20 2016 na klabu ya Al Ahly yaMisri kwa jumla ya goli 2-1, sasa wanajiandaa kurudi kucheza Kombe la shirikisho barani Afrika katika hatua ya 16.
Yanga imepangwa kucheza na klabu ya Grupo Desportivo Sagrada Esperançaya Angola katika hatua ya 16 bora ambapo mechi zitachezwa nyumbani na ugenini na baada ya hapo timu nane zitaingia katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Kombe la shirikisho barani Afrika, Grupo Desportivo Sagrada Esperançailianzishwa December 22 1976 .
gfd.jpg


Yanga ataanza kucheza nyumbani kati ya Mei 6-8 na mechi za marudiano zitachezwa kati ya Mei 16-18 2016

SOURCE: tanzamedia blogspot
 
nitapataje jezi ya Sagrada Esperanca ya Angola itakayocheza na yanga mwezi ujao
usiwe na mashaka, nalifanyia kazi hili sahivi, tutazitengeneza kwa wingi kabisa na kuziuza siku ya mechi hivyo andaa elfu kumi yako tu...hii huwa ni fursa nzuri sana ya kupata hela za mashabiki wa simba kama wewe....
 
Huko kwao hao jamaa wanashika nafasi ya kumi nasikia..
 
View attachment 341374

Baada ya kutolewa na Al Ahly kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika timu ya Yanga sasa kupambana na Esperanca ya Angola.

Utaratibu wa CAF ulikuwa kama ifuatavyo;

Timu nane (8)zilizofuzu kutoka michuano ya shirikisho ambazo ni Esperance (Tunisia), Stade Gabesien (Tunisia), FUS Rabat (Morocco), Misr Makkassa (Egypt), Esperanca (Angola), CF Mounana (Gabon), Kawkab (Morocco) and Medeama (Ghana).

Na timu nane (8)zilizofuzu kutoka ligi ya mabingwa ambazo ni TP Mazembe (DR Congo), Etoile du Sahel (Tunisia), El Merreikh (Sudan), Stade Malien (Mali), MO Bejaia (Algeria), Ahli Tripoli (Libya), Mamelodi Sundowns (South Africa) and Young Africans (Tanzania)

Image.ashx


Mechi hizo kuchezwa 6-8 Mei 2016 kwa mechi za mzunguko wa kwanza na tarehe 17-18 Mei 2016.

Kila la kheri Yanga.


Kwa mpira wa Yanga, tutasikia majigambo kibao magazetini kabla ya mpambano kuanza.....watatoka sare hapa Bongo na hawa wareno.....kisha wataenda kuzika maalbino Pemba kabla ya kwenda Angola kubebeshwa magunia ya magoli tena.
 
Huko kwao hao jamaa wanashika nafasi ya kumi nasikia..
Ndio wanashika nafasi ya 10 katika ligi yenye timu 16. Msimu uliopita wa 2014/2015 waliishia nafasi ya 10 ila wameshiriki kombe hili la shirikisho baada ya Kuwa mabingwa wa kombe la FA kule kwao. Tukijipanga tunaweza kuwatoa hawa jamaa, cha msingi timu yetu ifanye maandalizi kama tunakutana na timu kama Al ahly na sio kuwadharau hawa Waangola.
 
Utakufa na pressure kwa kushabikia timu mzigo lisilo kwenye ramani ya soka kimataifa[emoji12] [emoji13]


Hivi Yanga inatambulika kimataifa, toka lini? Hata ile mechi ya jana mtangazaji alikuwa hana uhakika Yanga inatoka wapi, watu wanajuwa Simba tu.
 
Msimamo wa Ligi kuu nchini Angola na nafasi waliyopo Hao wapinzani wetu kombe la Shirikisho timu ya Sagrada Esparenca

TABLES
League table Half-time Wide Form Over/under
Compare two teams
CAF Champions
League
Relegation
# Team MP W D L F A D P Last 5 matches H2H
1 1º de Agosto 7 6 0 1 16 5 +11 18
2 Desportivo Huíla 8 5 2 1 10 5 +5 17
3 Benfica Luanda 8 5 0 3 6 5 +1 15
4 Petro de Luanda 8 4 2 2 6 5 +1 14
5 Recreativo do … 7 3 3 1 12 10 +2 12
6 Kabuscorp 8 3 3 2 9 7 +2 12
7 Interclube 7 3 1 3 4 5 -1 10
8 Progresso Lund… 8 3 1 4 5 7 -2 10
9 Progresso 8 2 4 2 4 6 -2 10
10 Sagrada Esperança 6 3 0 3 6 4 +2 9
11 1º de Maio 8 2 3 3 9 13 -4 9
12 ASA 7 3 0 4 11 10 +1 9
13 4 de Abril do … 8 2 2 4 8 8 +0 8
14 Recreativo da … 8 2 1 5 6 10 -4 7
15 Porcelana 8 2 1 5 4 8 -4 7
16 Académica do L… 8 1 1 6 5 13 -8 4
 
Hivi Yanga inatambulika kimataifa, toka lini? Hata ile mechi ya jana mtangazaji alikuwa hana uhakika Yanga inatoka wapi, watu wanajuwa Simba tu.
Simba wale wa serengeti au wa wapi? Maana kama hamchezi mechi za kimataifa, mnatambulikaje sasa? Pamoja na kushindwa katika mechi hizo lkn tumecheza na tuliocheza nao wametukubali.

Ninyi mmecheza ngapi?
a00e8268f4a36f9fea0e6795eb8f0273.jpg


Ukiongeza ya jana ni 2-3 kwa mbinde
 
Back
Top Bottom