CAF yakumbushia comeback kubwa kuwahi kutokea ya Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika

Hili ndo lilikuwa jeshi lenyewe la kutuliza ghasia lililothibitishwa na shirikisho la soka Afrika (CAF)...!

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
 
Hili ndo lilikuwa jeshi lenyewe la kutuliza ghasia lililothibitishwa na shirikisho la soka Afrika (CAF)...!

Kulitaka Mwana Kulipewa MwanaView attachment 1416334
Mkuu Ghazwat umenikumbusha mbaali sana. Simba walishinda mechi ile mbele ya Rais Keneth Kaunda wa Zambia. Lilipo fungwa goli la nne Rais Kaunda akinyanyuka na kusindikizwa kwenye gari lake na kuondoka uwanjani. Alipokua anatoka getini akapewa taarifa kuwa wamepigwa bao la tano

Magoli yote matano yalifungwa na wachezaji wawili. George Kulagwa(marehemu) aliyefunga magoli mawili na Thuweny Ally(anaishi falme za kiarabu sasa hivi) aliyefunga magoli matatu

Baada ya mechi ile kwenye raundi ya pili Simba SC ikapangiwa kucheza na Union Sportive Douala ya Cameroon ambao ndio walikua mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Barani Afrika.

Ilikua ni miaka ya kusisimua saana. Wakati huo Yanga walikua wanachehemea tu katika nafasi
ya tatu kwenye ligi ya Bongo, maana waliokua wakishika nafasi ya pili na kupata fursa ya kushiriki Kombe la washindi barani Afrika(Cup Winners Cup) walikua ni Pan Africa ya pale Mtaa wa Swahili Kariakoo
 
Mungu akubariki mkuu. Nimekumbuka mbali sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu yenye rekodi mbaya ya aibu ya kufungwa au kutobolewa tungu Mara 3 mbele ya Rais, ya kwanza mbele ya mwinyi, ya pili mbele ya magufuli kagera sc 1-0, ya tatu mbele ya magufuli Yanga 1_0, wanunuaji wa marefa fc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Mkapa tutapindua meza,historia hiyo Simba tunayo,nia tunayo,sababu tunayo na hari tunayo.
Simba nguvu moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…