Mkuu Ghazwat umenikumbusha mbaali sana. Simba walishinda mechi ile mbele ya Rais Keneth Kaunda wa Zambia. Lilipo fungwa goli la nne Rais Kaunda akinyanyuka na kusindikizwa kwenye gari lake na kuondoka uwanjani. Alipokua anatoka getini akapewa taarifa kuwa wamepigwa bao la tano
Magoli yote matano yalifungwa na wachezaji wawili. George Kulagwa(marehemu) aliyefunga magoli mawili na Thuweny Ally(anaishi falme za kiarabu sasa hivi) aliyefunga magoli matatu
Baada ya mechi ile kwenye raundi ya pili Simba SC ikapangiwa kucheza na Union Sportive Douala ya Cameroon ambao ndio walikua mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Barani Afrika.
Ilikua ni miaka ya kusisimua saana. Wakati huo Yanga walikua wanachehemea tu katika nafasi
ya tatu kwenye ligi ya Bongo, maana waliokua wakishika nafasi ya pili na kupata fursa ya kushiriki Kombe la washindi barani Afrika(Cup Winners Cup) walikua ni Pan Africa ya pale Mtaa wa Swahili Kariakoo