CAF yamfungia maisha Refa Msaidizi, Marwa Range(Kenya) kujihusisha na Soka

CAF yamfungia maisha Refa Msaidizi, Marwa Range(Kenya) kujihusisha na Soka

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Africa(CAF) imewapa Marefa 11 adhabu tofauti kutokana na Makosa mbalimbali waliyoyafanya

Refa Msaidizi kutoka Kenya, Marwa Range amefungiwa maisha kujihusisha na shughuli zozote za soka zinazohusiana na Shirikisho hilo

Aidha, Refa msaidizi, Jallow Ebrima(Gambia) na Refa Yanissou Bebou (Togo) wamefungiwa kwa miaka 10 kujihusisha na shughuli zozote za soka zinazohusiana na Shirikisho hilo

Katika adhabu hizo pia, marefa wengine 8 wepewa adhabu ya kati ya miaka miwili hadi 6 kutokujihusisha na shughuli zozote za soka za Shirikisho hilo
Screenshot_2018-07-08-11-54-50-1.jpg
Screenshot_2018-07-08-11-54-58-1.jpg
 
Marwa alikula mlungula huyo. Na jamaa aliyempa rushwa alikuwa mwanahabari huku akijifanya ni Afisa wa chama cha soka. Alimrekodi video kwa siri pasipo mwenyewe kujua.
 
Marwa alijitia kidole mwenyewe
Na alikua ameitwa na Fifa kwenda
Urus
 
Marwa alikula mlungula huyo. Na jamaa aliyempa rushwa alikuwa mwanahabari huku akijifanya ni Afisa wa chama cha soka. Alimrekodi video kwa siri pasipo mwenyewe kujua.
alikula rushwa ili afanye kitu gani ile habari mpaka leo sijaielewa vizuri yaani aliyempa hela alitaka apate huduma gani?
 
Kumfungia maisha ni kumnyima haki ya kutubu ndio maana sipendi mpira wetu majungu mengi sana
 
Back
Top Bottom