JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Raundi ya Kwanza ya Michuano ya Afrika ngazi ya klabu inatarajiwa kuanza wikiendi hii ambapo timu za Tanzania pia zitakuwa uwanjani ndani na nje ya Nchi.
Leo Septemba 10, 2022, Yanga itavaana na Zalan ya Sudani Kusini kwenye Uwanja wa Mkapa, Simba ipo Malawi kucheza dhidi ya Nyasa Big Bullets.
KMKM ya Zanzibar itaikaribisha Al Ahli Tripoli ya Libya kwenye Uwanja wa Amaan, mechi zote zikiwa ni za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, kesho Septemba 11, 2022, Kipanga ya Zanzibar itakuwa Sudan Kusini kucheza dhidi ya Al Hilal Wau South, Geita Gold ikiwa ugenini kukipiga dhidi ya Hilal Alsahil ya Sudan.