Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Kauli hiyo imetolewa wakati ujumbe wa CAF ulipotembelea MOI kwa ajili ya kujionea uwezo wa taasisi hiyo katika utoaji wa huduma za afya, hususani katika maeneo ya mifupa, mishipa ya fahamu na majeraha yanayohusiana na michezo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja wa Huduma za Afya CAF, Bw. Boubakary Sidiki, amesema CAF imeridhishwa na maandalizi yanayofanywa na MOI, akisisitiza kuwa huduma bora za afya ni sehemu muhimu ya kuhakikisha usalama na ustawi wa wanamichezo wakati wa mashindano wakati wa mashindano hayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tiba shirikishi wa MOI, Dkt. Asha Abdullah, amesema MOI iko tayari kutumia utaalamu na uwezo wake kushirikiana na CAF, na wadau wa michezo katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo imara wa tiba za michezoni.
“MOI iko tayari kushirikiana na CAF, wadau wote kuelekea AFCON 2027. Tunaamini maandalizi haya ni fursa ya kuimarisha huduma za tiba za michezoni na kuhakikisha wanamichezo wanapata huduma bora, salama na kwa wakati,” amesema Dkt. Asha.
Amesema ushirikiano huo hautaishia kwenye AFCON 2027 pekee, bali utaendelea kuwasaidia wanamichezo, timu, vilabu na wananchi kwa ujumla kupitia kuimarika kwa utaalamu, vifaa, mifumo ya huduma na uwezo wa wataalamu katika tiba za michezoni.
Ukaguzi huo unaonesha nafasi ya MOI kama mshirika muhimu katika maandalizi ya AFCON 2027, huku ikifungua fursa ya kujenga ushirikiano mpana zaidi kati ya wataalamu wa afya, taasisi za michezo na wadau wa kimataifa.