beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Hati za Ukaguzi Zilizotolewa Katika Miradi ya Maendeleo Kwa mwaka 2019/20, CAG alikagua jumla ya miradi ya maendeleo 290 na kutoa aina mbill za Hati za Ukaguzi ambapo; alitoa Hati Zinazoridhisha kwa miradi 275 sawa na asilimia 95 na Hati Zenye Shaka kwa miradi 15 sawa na asilimia 5.
Hati Zinazoridhisha zimeshuka kwa asilimia 2 kutoka asilimia 97 mwaka 2018/19
Athari
Kushuka kwa idadi ya Hati Zinazoridhisha na kuongezeka kwa idadi ya Hati Zenye Shaka, kunaashiria kushuka kwa uwezo na uelewa wa Watumishi wa Idara ya Uhasibu waliopo katika
Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika kufuata viwango ya kimataifa ya wandaaji wa hesabu katika sekta ya umma a ripoti nyingine za fedha a Mamlaka ya Serikali za Mitaa
Aidha, udhaifu katika vitengo wya ukaguzi wa ndani, kukosekana au kutofanya kazi kwa kamati za ukaguzi wa ndani au kutokuzingatiwa kwa Sheria ya Ununuzi ya Umma hupelekea wahasibu kushindwa kuandaa hesabu kwa kufuata viwango ya kihasibu hivyo kushindwa kupata hati zinazoridhisha.
Madhara ya udhaifu huu ni;
1. Uwezekano mkubwa wa kupotosha watumiaji wa taarifa hizi, kutokana a tatizo la usahihi wa hesabu na ripoti nyingine za fedha.
2. Hesabu na taarifa za fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutoaminiwa na wadau na watumiaji wengine wa taarifa hizo, na Upotevu wa fedha a rasilimali za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kutokana na kuripoti mapato na matumizi yasiyo sahihi.
Ushauri
WAJIBU inaishauri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani (Internal Auditor General) pamoja na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora zifanye yafuatayo;
1. Kuwapa mafunzo ya mara kwa mara Watumishi wa Idara ya Uhasibu walioko katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwenye viwango ya kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta ya umma yanayotokea duniani.
2. Kuimarisha Vitengo wya Ukaguzi wa Ndani na Kamati za Ukaguzi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Hii ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wahusika wa uzembe utakaobainika kama njia ya kukomesha uzembe huo.
WAJIBU INSTITUTE