benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2021/22, imebaini katika Mamlaka 19 za Seri kali za Mitaa, , wanafunzi 23,009 wamekatisha masomo yao shule za sekondari kutokana na ujauzito, huku Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ikiongoza.
Katika shule za msingi, wanafunzi 19,945 hawakumaliza masomo kutokana na sababu hiyo. Ripoti hiyo, imebaini Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, inaongoza kwa wanafunzi wake kukatisha masomo wakiwamo 9,045, ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, walioacha masomo 2,172.
Kwa mujibu wa Ripoti Kuu ya Ukaguzi wa Serikali za Mitaa (LGAs) ya mwaka 2021/22, CAG Charles Kichere, alibaini wanafunzi wa sekondari waliokatisha masomo ni sawa na asilimia 28, kati ya 82,236 waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 па kutakiwa kuhitimu mwaka 2021
Kwenye ripoti hiyo, CAG ameeleza sababu za kukatisha masomo zilikuwa ni pamoja na ujauzito kwa wanafunzi wa kike, umbali mrefu kutoka makazi ya wanafunzi hadi shuleni, malezi ya familia na sababu binafsi. Ripoti hiyo inaonyesha kila halmashauri na idadi ya wanafunzi waliokatisha masomo kwenye mabano ni Kinondoni (4,652), Mji Newala (3,783), Misungwi (2,570), Morogoro (1,948) na Moshi (1,270). Nyingine Kilosa (1,246), Temeke (1,185), Buhigwe (908), Gairo (700) na Mpanda (691).
Shule nyingine ni Tandahimba (685), Kalambo (669), Mwanga (536), Busokelo (468), Newala (453), Kigamboni (426), Mji Masa-si (392), Makete (382) n Monduli (45).
Wakati kwa shule za msingi ni Gairo (1,365), Kwimba (9,045), Uvinza (2,172), Kilosa (2,096) na Nsimbo (1,545). Alizitaja nyingine ni Kibondo (1,416), Kibaha (806), Morogoro (641), Mwanga (460), Newala (345), Makete (54).
Kutokana na tatizo hilo, CAG alipendekeza kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), iandae programu za kuzifikia jamii husika, kuhimiza wazazi na walezi ku-waandikisha wanafunzi katika shule zilizo karibu.
Aidha, alipendekeza serikali za mitaa kujenga shule mpya karibu na vijiji, kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kwa kujumuisha vifaa vinavyofaa vya kufundishia na kujifunza, kuhimiza michezo na kutoa elimu ya taaluma na ufundi stadi.