Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Kwa tuliokuwa tunaulizia mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere ulipofikia, leo CAG ametoa majibu, hauna dalili ya kuisha, ndio kwanza umefikia asilimia 48, kwa hesabu za asilimia maana yake hata nusu haujafika.
Ujenzi wa mradi wa ufuaji umeme wa Mwalimu Nyerere ulianza mwaka 2019 na ulitarajiwa uwe umeanza kuzalisha megawati 2115 mwishoni mwa mwaka huu na kuendeshwa na TANESCO.
========
CAG: Kuchelewa kwa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere kwa asilimia 46.45. Hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2021 mradi ulipangwa kukamilika kwa asilimia 94.47, hata hivyo nilibaini mradi ulikamilika kwa asilimia 48.02 ukiwa umechelewa kwa asimilia 46.45.
=>Ucheleweshaji umesababishwa na kuchelewa kuwasilishwa kwa usanifu wa mwisho wa mradi, janga la mafuriko kwenye mto Rufiji pamoja na janga la Uviko.
=>Pia kukatika katika kwa umeme kwenye eneo la mradi kunasababisha kuongezeka kwa gharama na muda wa kukamilisha mradi.
Pia, soma=> Rais Samia apokea ripoti ya CAG, deni bado ni himilivu. Mafao yazidi mapato ya mifuko ya hifadhi