CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

Tanzania hakuna Watanzania wenye uwezo wa kupanda ndege kutokana na wengi vipato vyao kuwa vidogo sana. Hivyo kutegemea 5% ya population ya 60 millions wenye uwezo wa kupanda ndege ili ATCL iingize faida ni kujidanganya.
Mzee uttoh yuko sahihi kabisa, mashirika yote ya ndege huwa hayaleti faida ya moja kwa moja kwa taifa. Biashara ya ndege kama yenyewe huwa haiingizi faida, ila faida zake huja kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo safari hizo za ndege hufanikisha ndani ya nchi husika.
 
Huyo uttoh hapo amesema out of context, amekwepa hoja.

Kuweka kumbukumbu sawa.
-ATCL ilianzishwa mwaka 1977 (Hivyo imekuwa akifanya biashara kwa zaidi ya miaka 40 sasa).

-Ndani ya miaka mitano iliyopita serikali imewekeza zaidi ya Trilioni 2 (zaidi ya bilioni 2000) kwa kununua ndege mpya kwa cash ili kuiwezesha ATCL kutengeneza faida kubwa.

-Mwaka 2018 ATCL ilitangaza kupata faida ya zaidi ya bilioni 28.

-Kila mwaka, tangu mwaka 2018 mpaka 2020 ATCL imekuwa miongoni mwa mashirika ya serikali yaliyotangazwa na waziri wa fedha kuwa yanaipa serikali gawio.

-Mwaka huu CAG imesema kwa mwaka 2019/20 pekee ATCL imepata hasara ya zaidi ya bilioni 60, na kwa miaka mitano mfululizo ATCL imekuwa ikivuna hasara tupu, na hakuna mwelekeo wowote wa ATCL kuja kupata faida ikiwa mwenendo wake wa kisasa kiuendeshaji hautabadilishwa.

Tulitaka Uttoh ajikite kujadili hizo 'facts' kwanza kabla ya kudandia vioja vya kuokoteza kwa mataga.
Tulia wewe hujui kitu!!
 
Tanzania hakuna Watanzania wenye uwezo wa kupanda ndege kutokana na wengi vipato vyao kuwa vidogo sana. Hivyo kutegemea 5% ya population ya 60 millions wenye uwezo wa kupanda ndege ili ATCL iingize faida ni kujidanganya.
Mkuu BAK nimeongezea mambo mengine kwenye uzi, hebu fanya kurejea tena.!!!
 
TATIZO LA ATCL NI JINSI FEDHA ZA WANANCHI ZILIVYOTUMIKA BILA WELEDI KATIKA UWEKEZAJI WA JINSI NDEGE ZILIVYONUNULIWA NA SEQUENCING YA UNUNZI WA NDEGE HIZO!!!
 
Tanzania hakuna Watanzania wenye uwezo wa kupanda ndege kutokana na wengi vipato vyao kuwa vidogo sana. Hivyo kutegemea 5% ya population ya 60 millions wenye uwezo wa kupanda ndege ili ATCL iingize faida ni kujidanganya.
 
Dah.....yaani Sh60bn kwa mwaka! Hivi shule moja ya msingi nzuri kabisa inaweza kugharimu kiasi gani kujenga? Hizi 60bn zinaweza kujenga shule ngapi?

Au:
Hizi 60bn zinaweza kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wangapi....kuanza mpaka kumaliza (say kozi za miaka 3)?

JPM bana......mwanzo alianza na gia za kubana matumizi....

Kuna jamaa juzi tunapiga soga akaniuliza: "hivi SMU katika hizi shughuli za mazishi ya JPM mbona walikuwa hawaoneshi nyumba ya JPM?" Sikumjibu.
Ni shule za msingi Mia na 20 za kisasa kabisa aproximatily 500M kwa shule moja
 
CAG mstaafu mh Uttoh amesema hakuna shirika la ndege lolote duniani lililowahi kupata faida katika miaka ya mwanzo ya operations zake.

Kuhusu gawio mh Uttoh amesema dividend hutolewa baada ya biashara kupata faida na huamuliwa na bodi kiasi gani cha faida kigawiwe kama dividends
Uttoh amesema kwa uelewa wake ATCL haijawahi kulipa dividend kwa serikali, na kama kuna fedha ziligawiwa kwa serikali na ATCL hicho ni kitu kingine siyo dividend

CPA Uttoh amesema kimsingi mashirika ya umma hayapaswi kulipa dividend kwa sababu hayafanyi biashara na ametoa mfano UDSM wanalipa dividend serikalini kwa biashara gani wanaykfanya?!

Source: ITV kipindi cha Kipima Joto
Kwa hiyo zile bilioni 28 tulizotangaziwa na mmiliki wa nchi akisema ni faida ya ATCL haikusawa kweli?
 
BAK unaniangusha, yaani unaendekeza mambo ya from hands to mouth?

Mishahara itapanda kama tutazalisha kiwango cha juu na hakiji tu bila kutoka jasho...Imagine miradi yote ya kimkakati iishe mishahara si ita triple?

So far hayati alitahidi sana kwanza kupunguza inflation na deflation kwenye riba, kisha social service kama elimu na afya aliiongezea budget even three times mlitakaje? Aliigawa cake ya taifa kwa wemgi zaidi...Wafanyakazi Tanzania hawafiki hata 11% kisha wanachukua 60% ya budget...Aliilipa mishahara bila kuchelewesha hata sekunde na in a very sustainable way

Tuongeze tija ndiyo mishahara kuonhezeka iwe justified, otherwise tunafanya unyojaji kwenye population ya amabo hawajaajiriwa...Ubinafsi wa hali ya juu!
Mi nawaambiaga lakini hawanielewagi hawa watu. Tuna serikali likubwa wafanyakazi wa kuanzia watendaji wa kata hadi wa huko juu wote wanategemea kodi za wafanyabiashara. Halafu bado watu wanataka mishahara ipande kila mwaka, ipande kwa kodi zipi?
 
Dah.....yaani Sh60bn kwa mwaka! Hivi shule moja ya msingi nzuri kabisa inaweza kugharimu kiasi gani kujenga? Hizi 60bn zinaweza kujenga shule ngapi?

Au:
Hizi 60bn zinaweza kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wangapi....kuanza mpaka kumaliza (say kozi za miaka 3)?

JPM bana......mwanzo alianza na gia za kubana matumizi....

Kuna jamaa juzi tunapiga soga akaniuliza: "hivi SMU katika hizi shughuli za mazishi ya JPM mbona walikuwa hawaoneshi nyumba ya JPM?" Sikumjibu.
Nina jamaa yangu mjeda alienda kuzika kule ngoja nimuulize huo mjengo upoje
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mkuu kuna shughuli za kiuchumi hapa nchini? Si ndiyo hizo watu wanabambikiwa kodi kubwa na kuporwa mapesa yao benki. Wengi wanaamua ama kufunga biashara zao au kuhamia nchi jirani, Wakulima kudhulumiwa mazao yao au kulaliwa katika bei ya kuuza matokeo yake nchi haisogei. Kuna matatizo makubwa sana nchini na kama alivyosema former CAG Assad 60% ya Viongozi ndani ya Serikali uwezo wao wa kuongoza ni mdogo sana lakini wako humo kwa miaka chungu nzima kila siku ni wale wale!
Tunahitaji mabadiliko makubwa sana Nchini.
Msikilize mama hapa chini.

Mkuu BAK nimeongezea mambo mengine kwenye uzi, hebu fanya kurejea tena.!!!
 
Tulisema Sisi kwamba, Akili aloitumia CAG siyo yakwake Bali ni akili iliyonunuliwa kufanya watakacho wanunuzi wake
 
Kwa hiyo tutegemee faida baada ya miaka 100? Watanzania tulimuonya dikteta kwamba ununuzi wa ndege si kipaumbele cha Watanzania na biashara ni hasara tupu kama ASINGEKURUPUKA hiyo zaidi ya 3 trillions si ingeweza kutumia kuongeza mishahara ya Wafanyakazi nchini!?
Una mawazo finyu Sana, heri ungekaa kimya tu unge hesabika una hekima.
 
Back
Top Bottom