CAG: Vifo watoto wachanga vimeongezeka Mbeya

CAG: Vifo watoto wachanga vimeongezeka Mbeya

KwetuKwanza

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
82
Reaction score
150
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali amesema kuwa katika Mwaka 2021/22 aligundua uwepo wa ongezeko kubwa la watoto wachanga katika Mamlaka mbili ambazo ni Halmashauri ya Jiji la Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Katika Ripoti yake CAG anaeleza kuwa takwimu zimeonyesha kuwa kwenye Halmashauri hizo vilikuwa vifo 135 na vifo 49 kwa watoto wachanga 1000 waliozaliwa ambavyo viwango vikubwa zaidi kuliko lengo la vifo 30 kwa watoto 1000 wanaozaliwa kama ilivyoelezwa katika mpango wa 'one Plan III'

Aidha Ripoti hiyo ya CAG inaeleza kuwa kwenye Halmashauri 20, kulikuwepo pia na vifo vya watoto wachanga wapatao 6335 kwa miaka miwili.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa CAG aliweza kubaini sababu kuu za vifo vinavyotokana na uzazi ni kuvuja damu wakati wa kujifungua ambayo husababisha zaidi ya robo moja ya vifo, mtatizo ya shinikizo la damu wakati wa ujauzito, upungufu wa damu wakati wa ujauzito, kifafa cha mimba na magonjwa yanayohusiana na ujauzito.
 
Back
Top Bottom