CAG wa Usajili kwa Clubs za Simba na Yanga

CAG wa Usajili kwa Clubs za Simba na Yanga

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
Tunapoelekea nusu ya msimu mimi Mkaguzi Mkuu wa Sirikali.

USAJILI WA DUBE
Wanachama waangalie jambo hili wakiwahoji viongozi wao. Hizo Milion 700 za kumnunua Dube alikula nani? Tunapoangalia katika misimu ambayo Dube amechezea Azam ni minne. Ambapo ameibuka na magoli jumla 32. Wastani wa magoli 8 kila msimu. Je hakuna mchezaji wa tsh milion 200 anayefika hiyo idadi?

Hoja
Dube amekuwa akicheza matches chache kutokana na kuwa majeruhi.

Akili
Unamsajili mchezaji ambaye muda mwingi ni majeruhi kwa pesa nyingi kiasi hicho. Are you normal? Kwa nini unamsajili mtu ambaye unajua ni majeruhi?

Swali
Mpaka sasa Dube ameshacheza matches ngapi na amefunga magoli mangapi?

Tunahamia ukaguzi wa Usajili Mchezaji mmoja wa Simba.
 
Dube nadhani apewe MDA kama Mbappe,

Dube Kwangu ni mchezaji mzuri, mechi zilizopita dube ameonekana bado ni majeruh . Hopefully ata recover na WANANCHI tunamthamini.

: Simba haina mchezaji kwenye uwezo wa Dube mkuu
 
Mambo haya yanatokea kwenye boli, kina shevchenko, torres, radamel falcao, mendieta, juan Sebastian veron, alexis sanchez, di maria, hazard na wengine wengi.

Mbappe mwenyewe sasa hivi anapambana asiwe kwemye kundi hilo.
 
Yanga walidhani wamewakomoa Azam kumchukua Dube baada ya Azam kumchukua Feisal, mwisho wa siku yanga wamenunua mbuzi kwenye gunia
 
Sema Dube naye papara nyingi sana. Ningekuwa mimi ndiyo kocha wa Yanga, ningemchomesha mahindi mpaka siku itokee timu imeshinda goli nyingi au inacheza na timu dhafu, ndiyo nampa nafasi sasa ili aongeze uwezo wake wa kujiamini.

Nadhani ameathiriwa na presha kutoka kwa mashabiki. Alikotoka hakuwahi kukumbana na presha kama anayoipitia sasa.
 
Sema Dube naye papara nyingi sana. Ningekuww mimi ndiyo kocha wa Yanga, ningemchomesha mahindi mpaka siku itokee timu imeshinda goli nyingi au inacheza na timu dhafu, ndiyo nampa nafasi sasa ili aongeze uwezo wake wa kujiamini.

Nadhani ameathiriwa na presha kutoka kwa mashabiki. Alikotoka hakuwahi kukumbana na presha kama anayoipitia sasa.
Azam pale uwanjani walikuwa wanamfanyia Hujma asifunge.
 
Dube nadhani apewe MDA kama Mbappe,

Dube Kwangu ni mchezaji mzuri, mechi zilizopita dube ameonekana bado ni majeruh . Hopefully ata recover na WANANCHI tunamthamini.

: Simba haina mchezaji kwenye uwezo wa Dube mkuu
Mbape kwenye ligi anafunga dube hafungi kwenye ligi akipewa mpira anaanguka mwenyewe
 
Kacheza Azam misimu takribani mi nne, kafunga magoli 34, yani wastani wa goli 8 kila msimu.

Majeraha nayo ni ya kila mara.

Yanga walithubutu vipi kumsajili Dube wakamuacha Guede?
 
Mambo haya yanatokea kwenye boli, kina shevchenko, torres, radamel falcao, mendieta, juan Sebastian veron, alexis sanchez, di maria, hazard na wengine wengi.

Mbappe mwenyewe sasa hivi anapambana asiwe kwemye kundi hilo.
Rudisha Akili yako sehemu yake hao wachezaji uliowaolodhesha wote wamewahi kufanya makubwa na magoli ya kutosha ktk nyakati zao bora Dube hajawahi kufunga magoli 10+ ndani ya msimu mmoja alafu unamuweka kundi moja na malijendi are you crazy?Acheni siasa za simba na yanga John Boko wa sasa ni bora mala elfu kuliko Dube.
 
Dube alisajiliwa kama asset lakini kadri siku zinavyosonga anageuka kuwa liability. Kwangu Guede au Ngushi ni Bora kuliko Dube
Wazee wa Kuiga! Dube walimsajili Kama ku-revenge kuwakomoa AZAM, Kumbe hawajui revenge zina wenyewe! Azam wamevuna Fei na 'wazee wa kuiga' wakaondoka na galasa Dube 🤣🤣🤣 wakome kuiga iga!!
 
Back
Top Bottom