Calculator ya kodi ya gari TRA imepunguza thamani ya baadhi ya magari?

DidYouKnow

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,229
Reaction score
1,950
Mjomba wangu alinunua Audi Q7 ya 2011. Akalipa ushuru kama milioni 45 wakati huo kwenye mtandao wa TRA ikionesha ina ushuru wa milioni 43.

Miezi miwili baadaye gari hiyohiyo ukiingia kwenye portal ya TRA inaonesha ushuru wake ni milioni 21. Najiuliza mbona alitumia pesa nyingi sana? Mwaka wa kodi bado haujabadirika. Kulikoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wakisema gari ya 2011 ni model ambayo mpaka leo inatengezwa au yalitengenezwa 2011 tu?!?
Ninavyojua magari yanakuwa na models, kila model inakuwa na generation yake. Mfano IST ina generations mbili, 2002 hadi 2007 na 2008 hadi sasa hivi. Ndio maana IST ya 2002 haina tofauti na IST ya 2005, japo kunaweza kukawa na modification kidogo tu katika customisation.
 
Kwenye kikokotoo cha TRA anagalia hiyo gari wameikadilia CIF ya shilingi ngapi, kama wewe CIF yako itakua kubwa kuliko hiyo waliyokadilia wao basi kodi inakokotolewa upya kwa kutumia CIF yako na hivyo utalipa zaidi. Kama CIF yako itakua chini ya yakwao basi watatumia ileile yakwao.
 
Aisee ndo nimezidi kuchanganyikiwa!!! Sijaelewa kabisaa
 
Usicomplicate mambo sana just deal na year of manufacture...the newer the year the higher the price and vice versa is true
 
Labda kwa magari mapya, kwa used cars sio lazima kuwa hivyo. Gari ya 2007 inaweza kuwa ghali kuliko ya 2010.

Lakini pia kujua generations za magari sio jambo baya kwa mnunuzi.
Yeah ni kweli range rover sport HSE ya 2007 ni ghali kuliko ya 2010.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…