Mwandishi anapolinganisha Afrika na California hataki kutuonyesha kwamba California ipo hapo ilipo kimaendeleo kwa sababu ya watumwa kutoka Afrika na maeneo mengine ya dunia.
Kuna mambo kadhaa muhimu ya kujiuliza kuhusu hilo.
Jambo la kwanza ni shughuli za utwamwa zilikoma lini?
Jambo pili, ni eneo lililotoa watumwa wengi kuliko maeneo mengine dunia, eneo la Afrika ambalo linalinganishwa na California lilipata uhuru wake lini?
Jambo la tatu na la muhimu sana ni Afrika inafanya mambo gani na California inafanya mambo gani?
Kimsingi kama tunataka kuwa wakweli na kutumia akili katika kuona mambo ni wazi kuwa Afrika inaharibiwa na waafrika wenyewe. Na mambo hayo yako wazi.