KERO Call Centre Utumishi ni kichomi

KERO Call Centre Utumishi ni kichomi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mrsmaiko

Member
Joined
May 17, 2024
Posts
18
Reaction score
13
Ukitaka kujua hujui piga namba za kituo cha huduma kwa wateja, itaanza vizuri tu karibu utumish kituo huduma kwa wateja, kwa msaada wanaanza bonyeza namba kama 1 au 2 au 3.

Ukichagua namba ya huduma yako weka loudspeaker, italia mziki mpaka inakatika. Ni masikitiko tu. Mh. Ridhowani Kikwete hii namba ni maumivu.

Huna pahali pa kuuliza, unasubiri majibu zaidi ya miezi mitatu, minne. Mh. angalia hili, nakupongeza umewaasa sana maafisa utumishi kushughulikia masuala ya watumishi sio kukwamisha.

Hii huduma bora isiwepo watu wajue tu panda basi uje Dodoma, hapa nalia na kikokotoo bado huduma kwa wateja!
 
Hata ile ya white house huwa inaita tu haipokelewi. Sasa taasisi kubwa kama hizo mbona mnaweka namba halafu hata hampokei sim?
Wekeni maroboti yapokee hata usiku wa manane
 
Ifike mahala watu wawe wanaenda dodoma tu. Saa nyingine mtu huna hela ya kusafiri utoke bukoba hadi dodoma kuuliza tu majibu ya barua. unawaza kuulizia barua majibu yanachkua miez 3 mpaka 4. Ukipiga call center wanakuwekea nyimbo mwishowe wanakata wemyewe.tena wanakwambia kwa kingereza ?????
Kwanin wasitumie kiswahili?? Watumish gani wanatumia English?????
Wanakwambia your call is important tobus you will be placed to next available agent.ndio imeisha hio.
 
Kiufupi tuna huduma mbovu sana kutoka Kwa watoa huduma wa serikali nidhamu serikalini imeshuka sana watu wanaishi kimazoea mteja anaonekana taka taka uwe na Kero au ushauri bado tuna safari ndefu ya kufika na huu uozo unafika mpaka watendaji wa chini halafu tunategemea matokeo chanya ya kiutendaji Hali ya kuwa viongozi wenyewe Wapo Wapo tu
 
Ifike mahala watu wawe wanaenda dodoma tu. Kama hamuamini piga uone
 
Ishu ya huduma kwa wateja kwa Tanzania ni mbovu, sio serikalini tu. Yaani mteja hana thamani. Unashangaa kuna namba ya kuhudumia wateja lakin wateja wanabaki na kilio. Majuzi nilipiga sm kuulizia muamala ambao umekaa hewani zaidi ya siku 3, mtoa huduma anajibu kwa jazba 'Basi njoo Dar utapata kwa haraka'
 
Ishu ya huduma kwa wateja kwa Tanzania ni mbovu, sio serikalini tu. Yaani mteja hana thamani. Unashangaa kuna namba ya kuhudumia wateja lakin wateja wanabaki na kilio. Majuzi nilipiga sm kuulizia muamala ambao umekaa hewani zaidi ya siku 3, mtoa huduma anajibu kwa jazba 'Basi njoo Dar utapata kwa haraka'
Afya ya akili ni muhimu sana
 
Ukitaka kujua hujui piga namba za kituo cha huduma kwa wateja, itaanza vizuri tu karibu utumish kituo huduma kwa wateja, kwa msaada wanaanza bonyeza namba kama 1 au 2 au 3...
Inabidi wawatafute flex.co.tz wanajua sana hizo kazi
 
Back
Top Bottom