Sijui niseme nini mkuu GEZA, nina kawaida ya kufatilia sana thread zako zinazo zungumzia hulka ya jamaa hawa - tell you what? unawafahamu like back of your hand; yaani wakati mwingine wanafanya mambo ya kushangaza sana - masaa yote wanafikilia biashara tu, kwao utu ni secondary!! Alafu kibaya zaidi wana hulka ya kutaka kufitinisha watu, watu walio kwenda Sudan ya Kusini juzi juzi hapa, wanasema jamaa hawa wanataka kulifanya Taifa hilo kama koloni lao, hawataki watu wengine kutoka Africa Mashariki kwenda huko kufanya Biashara! Hulka hiyo wanaitumia vile vile nchini Rwanda we sema Mh Kagame pamoja na mapungufu yake yuko makini sana na jamaa hawa.
Nani kawambia OBAMA ni mjinga wa kuweza kurubuniwa ovyo na watu wapenda sifa na wapenda kutumia umaharufu wa OBAMA kwa madhumuni ya kuendeleza biashara zao na utalii, hawana uchungu wowote WA KWELI na OBAMA save wajaluo wenzake wa Nyanza; OBAMA anawajua vilivyo hawezi hata siku moja akasahau the late Mzee Jomo Kenyatta na administration yake ilivyo mdhalilisha baba yake mzazi - mzee OBAMA aliwahi kuambiwa na Kenyatta kwamba atahakikisha anasaga lami mpake sole ya viatu vyake inakwisha akitafuta kazi ya kuajiliwa - mzee wa watu alikufa a broken man na PhD yake ya ECONOMICS!!
Mkuu GEZA - self intuition ya Rais OBAMA unayozungumzia kuhusu watu hawa inatokana na mambo ya kinyama walio mfanyia BABA yake mzazi, Rais OBAMA hatakaa hata siku moja eti hayasahau na tuki add a salt to an injury kuhusu usanii uliyo tumika katika upigaji kura wa hivi karibuni nchini Kenya kwa kuhakikisha Mjaluo mwenzake haoni ndani, mbinu hizo za kutibua kura kimaksudi ndio kulimtibua zaidi Rais OBAMA - Administration ya Kenya wasijidanganye kwamba Rais OBAMA alikuwa hafatilii kwa karibu sana kilicho kuwa kinajiri katika kuhesabu kura.
Geza umenifanya nikaribie kuvunjika mbavu kwa vicheko uliposema walianza kujitayarisha kutagazwa kuwa jimbo la 51 la Merikani - wako radhi kusema lolote kama mbinu za kijitangaza Kimataifa, kama waliwahi kurubuni DUNIA kwamba Mlima Kilimanjaro huko nchini mwao kwa nini tushangae ya jimbo la 51 la MERIKANI kuwa Barani Africa! Oh yes, kwani Hawaii hiko umbali gani kutoka bara la Uncle SAM (U.S) - wanaweza kuja na hoja kama hii ku-justfy such a wild idea.
Mwisho nimalizie kwa kusema kidogo kuhusu business man wa Kenya ambaye alikuwa ana spit fire katika Radio ya BBC World Service, analalama kwamba kwa nini OBAMA hataki kupitia/zuru Kenya kwanza kabla hajaja TANZANIA, eti Tanzania hatuna lolote la maana zaidi ya mambo ya ujamaa na kijitegemea!! Yaani mawazo yake yako kwenye miaka ya sabini, sijuhi hata kama amewahi kutembelea Tanzania siku za karibuni; eti Tanzania hakuna wafanya biashara wa maana wa kuweza kuingia ubia na wafanya biashara kutoka Merikani!! As far as they are concern the WORLD is KENYA!! Masaa yote wako self centered TU na kajishahau kwamba anayo yazungumza Dunia nzima inamsikiliza akipwayanga na ngonjera zake zisizo na mshiko.
Nataka nieleweke kwamba binafsi sina tatizo na Raia walio wengi nchini Kenya, tatizo langu ni hawa wachache wenye hulka za ajabu ambao hawajui kabisa kuheshimu binadamu wenzao.