Camera za Usalama kufungwa Mlima Kitonga ili kudhibiti ajali

Acha uongo weka ushahidi hapa kama basi la Majinja lilipata ajali kitonga!?
 
hili ni la polisi na RC kwa suluhisho la muda mfupi na nafasi waliyopo,lakini sidhani kama ndio serikali kwa ujumla wake ifikie hitimisho hapa.

bado eneo hili linahitaji hatua kubwa zaidi ya hizi,kwa nyakati hizi tech imeshakua sana ni swala la kuweka pesa zaidi hiyo njia upunguzwe zaidi kona na barabara itanuliwe zaidi,lakini pia kingo imara zifungwe.
 
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."
Tatizo lililopo Mlima Kitonga ni kwamba ile barabara ni nyembamba sana, lane moja tu ya kupanda na lane nyingine ya kushuka. Barabara hiyo inatakiwa kupanuliwa kwa kuongeza angalau lanes zingine mbili ili kuifanya kuwa barabara ya lanes nne(4), mbili za kupanda na nyingine mbili za kushuka mlima, kuweka sehemu za kupumzika pembeni mwa barabara, pamoja na kuweka concrete road blocks katikati ya barabara ili kutenganisha magari yanayopanda mlima na yale yanayoshuka mlima ili kuzuia ajali za kugongana uso kwa uso. Aidha, pia unatakiwa kujengwa ukuta wa zege/ukingo au kujenga strong concrete retaining wall pembezoni mwa barabara hiyo ili kuzuia au kuyakinga magari yasiweze kuacha njia na kutumbukia kwenye ngema chini na kusababisha ajali, hata kama gari litaharibika au kufeli breki bado haliacha njia na badala yake litaendelea kubaki kwenye barabara yake.
Hilo ndilo suluhisho la kudumu ili kudhibiti ajali za barabarani za mara kwa mara zinazotokea hapo Mlima Kitonga, nimewahi kuona wametumia njia hii ktk nchi mojawapo niliyowahi kutembelea hapa duniani, bado naendelea na utafiti wa kuzipata picha za barabara hiyo, nikizipata nitaziweka hapa hapa mtandaoni ili watu wa TANRODS na TARURA pamoja na Makampuni ya ujenzi wa barabara waweze kujifunza kutoka kwa wenzao walioendelea zaiddi kwenye haya masuala ya ujenzi wa barsbara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…