Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Katika hali kuendelea kufurahi lakini ghalfa watu wanadondosha machozi na vilio vingi baada ya kupokea au kushuhudia mmoja wao anapata tatizo ambalo linampelekea kufariki dunia.
Sikia hiki kisa kutoka huko Cameroon
=========
Katika hali ya kushangaza Jumamosi ya Oktoba 26, bibi harusi aliyefahamika Kwa jina la Sorelle Manuella, alianguka ghafla na kuaga Dunia wakati sherehe za harusi zikiendelea huko Douala Cameroon, baada ya kupata mshtuko wa moyo.
Sorelle aliyekuwa akiimba kwaajili ya mume wake alianguka ghafla, huku wengi wakidhani pengine alikuwa anaigiza kuchangamsha watu waliojitokeza lakini baada ya kuwa kimya Kwa muda ndipo wakagundua kuwa amepata na matatizo, na haraka jitihada za kumuokoa zikaanza na baadaye kumuwahisha hospitali.
Baada ya kupelekwa katika hospitali mbili tofauti, taarifa za Madaktari zilionyesha kuwa sorelle ameaga Dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati sherehe hizo zikiendelea.
Sorelle ameacha mume na watoto watatu, huku mtoto wake wa mwisho akiwa na umri chini ya mwaka mmoja.
Soma Pia: Bibi harusi mtarajiwa, mama yake wafa ajalini wakielekea Kilimanjaro kwenye maandilizi ya harusi yake