Mchambuzi hutoa maoni yake kutokana na jinsi aonavyo. Hata ukicheki wachambuzi wa sky sport nao hutoa predictions zao nao pia huingia chaka vile vile.
Kama neno lenyewe Uchambuzi lilivyo ni maelezo au kuingia kwa kina ndani ya jambo fulani ambalo either limetokea au linaenda kutokea. Na katika mabo kama hayo kuna kupata na kukosea.
So msimuandame sana, sio mpiga ramli. Cheki hao waliocheza mpira kina Kuffor, Carregher, Neville na wengine wanavyopwaya sometimes.
Tena kwa case kama ya cameroon yani kwa mtu makini asingepishana na Kumwembe, ukiangalia hali halisi Cameroon kwenye mashindano haya hana kile kikosi ambacho kimezoeleka miaka mingi chenye majina ya wanaotamba kwenye ligi kadhaa kubwa duniani, ila wana timu nzuri inayoshirikiana kitu kinachowapa matokeo. sina hakika kwamba kuna kundi kubwa la wadau walioipa cameroon nafasi kubwa at expense of Ghana, Ivory coast na Algeria.