Camouflagers na informers

Camouflagers na informers

Hapo vipi
samaki%20pic.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ngumu sana
Unaweza hata kumkuta akijifanya chizi maarifa
Muuza urembo
Mwalimu
Fundi nknk kulingana na nature ya kazi...

Jr[emoji769]
Dah! Jibu limeni disappoint Sana hili asee...wewe sio wa kunijibu kwa Mizunguko hivi...nilitegemea angalau unipe hints chache za kunifungua macho, masikio na ubongo kidogo...ila fresh baridaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah! Jibu limeni disappoint Sana hili asee...wewe sio wa kunijibu kwa Mizunguko hivi...nilitegemea angalau unipe hints chache za kunifungua macho, masikio na ubongo kidogo...ila fresh baridaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mmh inaelekea una majibu yako tayari kichwani ama pengine ulitegemea nikutajie kwa majina?

Jr[emoji769]
 
Mmh inaelekea una majibu yako tayari kichwani ama pengine ulitegemea nikutajie kwa majina?

Jr[emoji769]
Nahitaji kujifunza mkuu, unajua elimu Hiyo ni pana na adhimu. Na yumkini ni elimu iliyo nje ya mitaala yetu hii ya kawaida. Hivyo ninapoona elimu Hiyo Au mtu mwenye maarifa kidogo kuhusu Habari hizo shauku ya udadisi hunipanda kama Mori, na sio vinginevyo boss.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahitaji kujifunza mkuu, unajua elimu Hiyo ni pana na adhimu. Na yumkini ni elimu iliyo nje ya mitaala yetu hii ya kawaida. Hivyo ninapoona elimu Hiyo Au mtu mwenye maarifa kidogo kuhusu Habari hizo shauku ya udadisi hunipanda kama Mori, na sio vinginevyo boss.

Sent using Jamii Forums mobile app
Poapoa ila kiukweli hao watu hawana alama wala mavazi maalum kiasi cha kuweza kuwatambua kwa urahisi na ni watu wa kila kaliba katika jamii

Jr[emoji769]
 
Only intelligence specialists can figure that out. Ila kwa mtanzania wa kawaida kama mimi, never ever
inawezekana.... kama una tabia ya kuwasoma watu na machale... kuna mtu nilimuhisi na nikajua ni Intel kutokana na tabia zake mtu mwngne angeona kawaida but nilitia Shaka uongeaji wake, kupotea potea ghafla na kufosi uchangamfu
 
Yuko mmoja overseerer wa wauza magenge hapa Nanjilinji alifanya kila linalo wezekana kuunga urafiki na mimi nikawa nimemstukia kiaina mapema sana. Nikamleta karibu ili asipate taabu kufanikisha alichokitaka kwangu.

Akawa best rafiki na jamaa yangu. Si kuwa na hofu maana mimi ni raia mwema daraja la juu kabisa(raia mkureshi tuseme hivyo). Mahusiano yetu yakawa ni nipe ni kupe, Kila nikipata habari yenye uzalendo ndani yake naianzishia stori tukiwa naye.

Kama jamaa au rafiki kahitilafiana na sheria na yuko mahabusu polisi akihitaji dhamana na mtanguliza yeye mbele dhamana inatoka chapu chapu Siku hizi ni marehrmu RIP nimekosa huduma na company yake. Ila nidhamu yake ilikuwa ya kupigiwa mfano na alikuwa wa msaada kweli.
 
Nimekua na rafiki yangu kwa muda mrefu kidogo, bahati mbaya ni yatima.Nimesoma nae advance huko pomerini iringa. Alikua mtu wa kusoma sana novel,alikua na kipaji cha kushawishi mnoo, yani akikaa na wewe ukawa unaamini katika jambo flani,basi akianza kujenga hoja lazima mwisho wa siku unakubaliana nae,kimsingi ana sifa za kipekee sana,ni mkimya kama mimi, but ukimya wake nilikua nauona kama sio ukimya as ukimya tu!

ila alikua kama ni mtu anaechakata vitu flani katika akili yake,ofcoz ni miongoni mwa watu wenye iq kubwa kuwahi kukutana nao,digrii yake kasoma sauti mwanza, na misimu yote akiwa anasoma pale nilikua nakutana nae sana tu, ingawaje kuna vipindi kadhaa naeza kuwa kwenye mihangaiko mikoa mingine ghafla nakutana nae stand, ukimuuliza anakwambia natoka kwa shemeji yako sehemu flan (mkoa).na kwakweli huyu bwana alikua mtu wa totozi sana. aliwahi kufanya field office mbili za mambo ya kisheria na mabosi wote wa office zile ni wanawake na alifanikiwa kuwanyanyua (Fu£$%&),nilikua namuuliza unawezaje kufanya hivyo?

alikua ananijibu tu,ni kazi rahisi sana ,moja kati ya vitu vilivyokua vikinishangaza ni lifestyle yake,hakua mtu wa kupata shida ya kipato kabisa, nilikua nikimchunguza sana mienendo yake lakini sipati jibu. Baada ya kumaliza chuo mwaka mmoja mbele nakuja kukutana nae morogoro. akanipeleka kwake katika appartment flan ni mkabala na fieldforce morogoro, alikua vizuri sana. usafiri mzuri nk.nk nikamdadisi lkn majibu mafupi tu.

kilichotokea baada ya hapo ni kwamba yule bwana hakutaka mawasiliano na mimi tena,ila ni baada ya kumchana kwa kumwambia nimekuelewa wewe ni nani. nikafuta na namba yake...
 
Back
Top Bottom