Nimekua na rafiki yangu kwa muda mrefu kidogo, bahati mbaya ni yatima.Nimesoma nae advance huko pomerini iringa. Alikua mtu wa kusoma sana novel,alikua na kipaji cha kushawishi mnoo, yani akikaa na wewe ukawa unaamini katika jambo flani,basi akianza kujenga hoja lazima mwisho wa siku unakubaliana nae,kimsingi ana sifa za kipekee sana,ni mkimya kama mimi, but ukimya wake nilikua nauona kama sio ukimya as ukimya tu!
ila alikua kama ni mtu anaechakata vitu flani katika akili yake,ofcoz ni miongoni mwa watu wenye iq kubwa kuwahi kukutana nao,digrii yake kasoma sauti mwanza, na misimu yote akiwa anasoma pale nilikua nakutana nae sana tu, ingawaje kuna vipindi kadhaa naeza kuwa kwenye mihangaiko mikoa mingine ghafla nakutana nae stand, ukimuuliza anakwambia natoka kwa shemeji yako sehemu flan (mkoa).na kwakweli huyu bwana alikua mtu wa totozi sana. aliwahi kufanya field office mbili za mambo ya kisheria na mabosi wote wa office zile ni wanawake na alifanikiwa kuwanyanyua (Fu£$%&),nilikua namuuliza unawezaje kufanya hivyo?
alikua ananijibu tu,ni kazi rahisi sana ,moja kati ya vitu vilivyokua vikinishangaza ni lifestyle yake,hakua mtu wa kupata shida ya kipato kabisa, nilikua nikimchunguza sana mienendo yake lakini sipati jibu. Baada ya kumaliza chuo mwaka mmoja mbele nakuja kukutana nae morogoro. akanipeleka kwake katika appartment flan ni mkabala na fieldforce morogoro, alikua vizuri sana. usafiri mzuri nk.nk nikamdadisi lkn majibu mafupi tu.
kilichotokea baada ya hapo ni kwamba yule bwana hakutaka mawasiliano na mimi tena,ila ni baada ya kumchana kwa kumwambia nimekuelewa wewe ni nani. nikafuta na namba yake...