Camouflagers na informers

Camouflagers na informers

KISWAHILI ni wazugaji na wafichua habari
Ni watu maalum lakini wa kila jinsia umri na kaliba... Kati yao wapo mpaka wezi matapeli, wakabaji na wachawi.. Lakini kila walipo wapo kwa lengo maalum.... Kutoa taarifa ambazo zitasaidia kubaini waovu na kuzuia hatari ama kulinda usalama wa nchi raia ama viongozi....
Hawa watu hutumika kwa namna tatu
1. Kutoa taarifa muhimu za kihalifu zinazosaidia kuepusha janga fulani katika jamii... Iwe la kiongozi ama jumuiya
2.Hutumika kuwajenga viongozi na propaganda za kukubalika kwa kiongozi fulani katika jamii
3. Hutumika wakati wa hatari ya usalama wa nchi,mipango ya mauaji ya viongozi, mapinduzi ya kijeshi, maandamano migomo nk
Ni aina ya watu wenye elimu na waliopewa mafunzo maalum juu na namna ya kuvaa uhusika fulani bila kujulikana, namna ya kuongea, kuripoti na kutoweka eneo la tukio bila kuacha alama yoyote na kujulikana uhalisia....

Mfano wa kwanza
Kiongozi mkubwa anapotaka kutembelea eneo fulani, wazugaji na watoa taarifa za siri hufika wiki moja ama zaidi kabla ya ziara rasmi... Hapa hujigawa katika makundi mawili
. kundi la kwanza ni la kusoma hali ya hewa kiusalama na kukubalika kwa kiongozi.. Mambo mabaya yanayotendwa na viongozi wa eneo husika na maoni ya wadau
. kundi la pili ni wazugaji. Hawa ni wana kitengo cha propaganda ili kuonyesha kukubalika, kuaminika na kuungwa mkono kwa kiongozi na imani juu ya wale aliowatembelea.. Hapa si ajabu kumkuta kiongozi anakula chakula mtaani kwenye banda fulani bila hofu, kunywa kinywaji kama dafu ama kula kitu kama karanga tunda nk... Wauzaji wa vitu vyote hivi ni watumishi wake waaminifu

Mfano wa pili
Nchi inapopitia kipindi cha mashaka kama maandamano usaliti na mapinduzi..
Hapa huangaliwa kwanza maeneo yenye ushawishi mkubwa wa jambo husika.... Ndipo hupelekwa timu ya watu maalum!! Mfano anafika mtu wa kawaida kwenye bar ya kawaida mtaani, ambapo pembezoni kuna kijiwe na bodaboda nk.. Huyu aliyeko bar anakuwa busy na simu na kinywaji chake... Hana story na mtu... Kisha anakuja mwingine mzugaji kama machinga, anajifanya anauza keyholders kwa bei poa sana na kama huna hela anakukopesha...
Bila kujua zile keyholders zina mawasiliano ya moja kwa moja na jamaa aliyeko pale bar

Mfano wa tatu
Hatari ya kuvamiwa kijeshi... Hapa ni pakubwa na penye mengi lakini wanawake warembo hutumika sana kipindi hiki... N kundi lingine ni wazugaji wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa na watafiti wanaotaka kuwekeza ama kutafiti....
Yote kwa yote jihadhari sana na mikusanyiko yenye dhumuni la maandamano hasa ya kisiasa ama kupinga jambo fulani kitaifa... Ukiachana na wale askari wa fanya fujo uone wenye mabomu ya machozi na risasi za mpira, huwa kuna mdunguaji mmoja tu hatari sana kwa ajili ya kumdungua kiongozi ama walio mstari wa mbele... Kimbia jifiche....

Unaposikia kiongozi kafika mahali na watu fulani wamewajibishwa kwa haki, tambua wazi ni kazi iliyotukuka ya wazugaji na wafichua habari
Unaposikia maandamano, mgomo ama mapinduzi fulani yameshindikana jua fika kwamba kuna kazi kubwa imefanywa na hawa jamaa
ILA unapoona mojawapo kati ya hayo niliyotaja yamefanikiwa vizuri, basi hawa jamaa ama wamefeli ama wanekengeuka miiko yao..!
Kamwe usiwaamini hawa watu hata kama ni ndugu yako... HAWATABIRIKI...!



Jr[emoji769]
Kwa Tanzania hawa watu jinsi wanavyofanya kazi zao ni kama SHILAWADU tu, hawana lolote la maana.
 
mimi nilishuhudia kuna jamaa ALIKUWA ni bodaboda ananichukuaga home ananipeleka kazini na kunirudsha pia, ...kuna siku alitukanana na demu mmoja ivi ambaye alimtongoza mara kwa mara afu demu anachomoa, jamaa alimtukana sana na demu pia alimtukana hadi hatua ya kutaka kupigana lakin watu waliokoa hilo, sasa ikafika mida ya sa kumi na moja jion mana waligombana mchana, yule demu akaja na kikosi Cha watu, afu akakaa pembeni , wale jamaa waliokuja na Demu wakaenda kwa yule mshikaji bodaboda wakamshika wakasema wao ni police na wanataka wampeleke kutuoni jamaa aliomba kuoneshwa kitambulisho ili kuamini ni police lakini walimtia pingu na kumpeleka kwenye gari yao aina ya Alphad , wakaingia humo ndani baada ya mda kama dk5 Tukaanza kusikia makelele ndani ya gar watu wakafika milango ikafunguliwa na waliokuwamo ndani, .... ase wale jamaa walitoka wameiva wamechapwa balaaa kumbe jamaa alikuwa ni mwanajeshi siku zote hizo hakuna aliekuwa anajua, ...walipomfungulia pingu jamaa akawapakia kwenye hilo gari lao na kumbeba na demu.... sijawah kumuona huyo jamaa mpaka leo ase ...

hivyo naamini katika post yako
Nionee huruma Mimi
 
Jamaa anajionaga ni next level kumbe ni kolo tu
Screenshot_20240526_075054_Gallery.jpg
 
🥺🤔🙇🏿‍♂
 

Attachments

  • IMG-20240617-WA0123.jpg
    IMG-20240617-WA0123.jpg
    63 KB · Views: 8
Back
Top Bottom