Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Just think for a second; Mojawapo ya lawama kubwa dhidi ya uongozi wa Nyerere ni kuwa hatukuwa na TVs, magari bwelele n.k n.k kwamba kulikuwa na uhaba wa vitu vingi.
Alipokuja Mwinyi na sera ya Ruksa basi vitu vikaanza kujazana maduka yakafurika na mitumba ikaruhusiwa kwa kasi kubwa na kusababisha Urafiki, Mwatex, Mutex n.k kukosa soko. Tukawa tunaingiza vitu vingi vya kigeni na kuvifurahia.
Na hata alipokuja Mkapa ndiyo ikawa zaidi kabisa tukafika mahali ya kuuza kama njugu mali zetu na kutafuta "wawekezaji" katika ile sera maarufu ya "ubinafsishaji" a.k.a "ujinasfishaji". Tukafika mahali hadi mazuria, samani, madirisha na mapambo ya ofisi zetu tukawa tunaagiza toka nje huku tukijivunia ni kutoka "Oman" (Al-Adawi ana kampuni kubwa ya mambo haya) na wengine tukiagiza vitu toka China.
Katika mwelekeo huo tumefikia mahali mjasiriamali wa Bongo akitaka kutengeneza clothline lazima ale mitkasi na watu wa China;
katika kufanya hivyo, tumefikia mahali tunaita tunachokiona kuwa ni "maendeleo"!
Sasa, swali langu which is a little bit political as well as philosophical ni kuwa nchi inaweza kuendelea kwa kuimport vitu kutoka nje na kuviita maendeleo? Je, endapo kwa mfano, hali inakuwa ngumu huko kwa wajomba, computer haziji, samani hazitengenezwi kwa kiasi cha kutosha, vyuma chakavu havinunuliwi, n.k n.k JE, Tanzania inaweza kujitegemea kuzalisha vitu vya maendeleo?
Tunapofikia kuwa hata masoko yetu ya kifahari yanaagiza hadi vitunguu kutoka nje, nyanya na mbogamboga toka nje, na sisi tunafurahia kwa sababu tunavyo vya kizungu au vya kisasa tunaweza kuita haya ni maendeleo?
Ni vifaa gani vya kompyuta tunavyozalisha wenyewe kama vipuri? Ni vifaa vya kiasi gani vya mashine mbalimbali tunavyozalisha wenyewe?
Ni kwa kiasi gani (kiasilimia) tuweze kufika mahali tunasema kuwa tunajitegemea kwa kiasi kikubwa?
Je maendeleo ni maendeleo kama yanategemea kuendelea kwa watu wengine!?