Nina maoni pacha na Joka Kuu kuhusu EAC.
Nimekuwa nikisema hivyo, Smatta anasema ni uchochezi. Kenya ndiyo iko mstari wa mbele kuhakikisha Federation inatokea, nyuma yake wapo jirani zetu wenye matatizo yale yale, nasema sitaki kulazimishana kuungana. Tulishakataa! Niko tayari kwenda vitani kukataa Muungano huu. Tunaweza kusaidiana hivi hivi tulivyo, hata sasa hivi Kenya chakula wananunua Tanzania, inatosha, maana njaa kali kule. Au basi wale viwanda vyao. Kuhusu Maji ya mto Nile, hatuhitaji kuungana kudai haki za mto huo.
Maji watu watumie kwa raha zao, Misri wakija kwa ubaya tutawachapa pamoja. Misri hana uwezo wa kupiga nchi zote hizo, vita ya sasa hivi si hela tu. Kama taleban wanawatoa jasho Marekani na madege yao, itakuwa Misri. Kisha kila mtu akae kwake. Viongozi wanaowasaliti watanzania watakwenda na maji. Mpaka sasa TZ imejitolea mambo mengi sana kwa majirani zetu, but they keep demanding.
Tumechoka na ma-free riders, na bahati tuna nchi kubwa na wakarimu, sijui wangekimbilia wapi. Kila anayekimbia njaa au vita, break ya kwanza ni Tanzania, mpaka lini. Sasa hivi kuna climate change, we need be careful. Wakiambiwa kuungana kwenye IGAD, hawataki, kwa vile hailipi, maana kuna Somalia na Ethiopia na kote njaa kali.
Siwaombei mabaya jirani hawa, ila they are burden to us. Kuendelea si mpaka ardhi kubwa, wakae kwao wafanye innovations, they can irrigate their barren land with proper technology and resources in place instead of thinking flocking to Tanzania, which is weak! Wawe wabunifu, kisha sisi tupange mipango ya matumizi sahihi ya ardhi yetu kwa kujifanasi. It's about comparative advantage. Wengine hata ardhi wanayo, but they chose to grab. Kwani Uswiss na Ujapani wana ardhi kubwa? Lakini wako juu. Ni mipango tu.
Si wanasema wamesoma, maana ya kusoma ni kuwa mbunifu na kutatua matatizo ya nchi yako, kuliko kuhamishia matatizo yako kwa wengine.