Elections 2010 Can REDET poll claims be trusted?

Hakuna utafiti uliofanyika wao waendelee kumdanganya tu Kikwete kwa uzuri wa sura watakuja shangaa watu wanazidi kutokuwa na imani naye wao wanasema anazidi kupendwa migomo imepamba moto wao wanasema utendaji wa serikali umeongezeka sijui ni serikali ya wapi wanayoisema yangu macho come to election day.
 
Kui amini au la itategemea kama methodology waliyotumia nayo unakubaliana nayo au la! Kwa hivyo kabla ya kujadili results angalia kwanza methodology!
 
Kui amini au la itategemea kama methodology waliyotumia nayo unakubaliana nayo au la! Kwa hivyo kabla ya kujadili results angalia kwanza methodology!

Mods: Unganisha hii topic imejirudia
 
Hili jambo niliwahi kulisema nyuma kuwa ni questionable. Kwani hizi poll inategemea wanauliza maswali gani? wametumia methodology gani? na Sample size yao.

Sasa kusema la haki kuinterview watu 1000 bila ya kusema selection ya hao watu ni kwamba inasababisha sample selection bias which affects the estimations coefficient na results in general. Pia tukija katika maswali kuna kitu kina ring questions mfano unamuuliza mfano mfanyakazi kuwa bosi wake huyu ni mbaya au mzuri? ni obvious atakujibu mzuri au unamuuliza mwanaccm je Kikwete unamuonaje?

Unadhani watakujibu vp?

So mie binafsi hizi study naziona ni uzushi na propaganda za kufanya watu waamini kuwa CCM inakubalika basi
 
Kui amini au la itategemea kama methodology waliyotumia nayo unakubaliana nayo au la! Kwa hivyo kabla ya kujadili results angalia kwanza methodology!

You very right. Kwanza kwa kuangalia juujuu inabidi hata uulize what are the obejectives of their polls? are they doing these polls for specific purposes, for fun, just a way of getting donor funds or for what. What is the make up of the team, who are they affiliated to. And we can as well ask ourselves,is Redet partisan or not (in my opinion it appears to be so).

Kwanini polls zao zinalenga mambo ya siasa tu, na haziangalii mambo ya msingi kabisa kwa mtanzania. Are they doing things in western way to justfy their presence to donors, huku wakiacha yale ya msingi wanayotakiwa kuyafanya kwa ajili ya watanzania.

Naona REDET ni mradi tu wa kuingiza pesa, we can ot for sure trust them.
 

duhu, kama wasomi wako hivi. tutetegemee nini?
Sasa kama huna la kufanya umeleta hapa ili iweje?
Mi najua kama ulimshukuru Mungu maana yake ulisamehe toka moyoni,its wonderful unakuja hapa kulalama tena!
Mean what you formely said broda!
 
[video]http://www.eastafricantube.com/media/31265/Asha_Ngedere/[/video]


 
Hivi hawa REDET mbona wako kimya kuhusu umaarufu wa wagombea wetu mwaka huu 2010? Mbona 2005 walifanya utafiti na walitoa matokeo ya utafiti wao?
 
Matokeo ya utafiti wa kura za maoni uliotolewa juzi na REDET(Research and Education on Democracy) kuwa CCM watashinda kwa 71.2% wakifuatiwa na CHADEMA 12.3%,CUF 10.3% yanadhihirisha kuwa CCM wanawatumia REDET kuwashawishi Watanzania kuwa bado wana kubalika waktiukweli wenyewe hauko hivyo.

Matokeo haya yamekuja wakti bado watu wanatafakari yale matokeo ya kura za maoni yaliyotolewa na Synovate ambao nao wanatuhumiwa kwa kuchakachua matokeo halisi ya kura za maoni ili kui-favour CCM baada ya Synovate kukumbana na ukweli halisi wapinzani wakiongozwa na CHADEMA ndo wanongozae kwenye maoni ya uchaguzi wa Urais kwa mwaka huu wa 2010!

Hii imedhihirisha kwamba matokeo haya ya kura za maoni(poll opinions) ni ya kugushi ili kuwafurahishi CCM na kuwaweka kwenye nafasi ya ushindi baada ya 31 Oktoba. Kwamba CCM watafanya kila mbinu kupindisha matokeo ya uchaguzi ili wapinzani wakilalamika REDET na Synovate watumike kama cover ya kuficha wizi wa kura!!!

Maoni ya REDET na Synovate ndiyo yakayotumiwa kama kigezo na JWTZ kuwadhibiti wapinzani kuwa LAZIMA WAKUBALIANE NA MATOKEO KWA SABABU REDET NA SYNOVATE walitangaza hivyo hata kabla ya Uchaguzi.

Hii ndiyo janja ya CCM kwa mwaka huu wa kutumia taasisi hizi kama kigezo cha kuwa-fool Watanzania kuwa pamoja na ukweli kwamba Wapinzani wanaonekana kukubalika kwenye Kampeni zao bado chaguo la watu ni JK na CCM.

If you think critically about these opinion polls utaona kwamba hawa jamaa wa Redet na Synovate wamefanya utafiti wao kwenye maeneo ambayo ni ngome za CCM. Kwa maana ya kwamba waliowahoji katika kutoa maoni yao aidha ni viongozi wa CCM au Wanachama /Wakereketwa wa CCM. Unapofanya Research huwezi ku-base kwenye eneo moja lenye ushabiki wa kitu unachokifanyia utafiti. Lazima ufanye random research kwa watu wa aina zote wenye sifa za kupiga kura.

Naamini kabisa hawa jamaa leo hii na hasa Redet wakiambiwa watoe orodha ya aina ya watu waliowafanyia mahojiano watakuwa ni wale wale wana-CCM kwa maana ya Makada,Viongozi na Wanachama wa CCM. Kama umepanga kuhoji watu 10 ili upate maoni yao kuhusu Uchaguzi wa mwaka huu, na ukaenda eneo la CCM kwa maana ya Kiongozi wa Kitongoji au Balozi lazima kaya 7 zitasema CCM wanafaa. Hii ni asilimia 70 kwa mahesabu ya chapchap.

Naamini kama Redet naamini kama
wangelifanya utafiti wao hapo Chuo Kikuu wanafuzni wakiwepo wasingepata hiyo 71.2%
Benson Bana na Mukandara wameshinikiza UDSM isifunguliwe ili waweze kutengeneza mazingira ya ushindi wa kishiindo wa Chama Twawala-CCM.

Na hii yote ni kutaka kujikomba kwa Kikwete ili atakapoingia Ikulu awakumbuke katika ufalme wake kama ilivyokuwa kwa Prof. Beno Ndullu ambaye kwa sasa hivi ndiye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Ni aibu kwa wasomi mahiri kama Prof.Mukandara na Benson Bana( Bunsen Burner) kuudanganya umma wa Watanzania kwa maslahi yao binafsi na CCM.

Mimi nataka niwakumbushe kile alichokisema Msajili wa vyama Mhe.John Tendwa kuwa WAPINZANI MWAKA HUU WANAWEZA WAKASHINDI VITI 80 VYA UBUNGE AU ZAIDI YA HAPO WAKIJIPANGA VIZURI.

Kwenye Bunge lenye jumla ya viti 250 vya Ubunge viti 80+ si ushindi mdogo. Hii kwa hesabu za haraka haraka ni zaidi ya asilimia 32+.

Lakini hebu tusubiri hiyo tarehe 31 Oktoba,2010 tuone nani msema kweli kwa sharti kwamba CCM wadhibitiwe wasije iba na kughushi matokeo.

Slogan ya Leo: TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA. Chagua SLAA,CHAGUA CHADEMA. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.Ameeeen!
















.
 
hawana lolote atudanganyiki na uchakachuaji huo wasubiri 31 october
 
Nina mashaka sana na matokeo ya utafiti wa REDET. Sina hakika kama matokeo ya utafiti wao yametolewa kama yalivyopatikana. Hatahivyo naomba tusiyazingatie sana. Tujitokeze kupiga kura hiyo tarehe 31October kwani ni kura tu zitakazo amua nani mshindi.

Mugisha
 

Hoja nzuri, ungeijibia kule kwenye forum ya Uchaguzi 2010 ingekuwa vema zaidi. Anyway, kwakuwa ni mgeni haina shida, mwanzo mzuri.
 
Wanajamii wote, kumbe tafiti za REDET na Synovate hufanyika kihuni sana.

Report zao zinaonesha kua walihoji watu moja kwa moja kwa kuwauliza maswali, wengi wa watu vijijini ni waoga. Walioenda kukusanya data wangewapa maswali bila kuandika jina pia wangeweka mazingira kama ya uchaguzi. Wengi ukiwahoji watakwambia CCM huko vijijini lakini kupiga kura wanabalisha kwa sababu hawaonekani na mtu yeyote. Kwa hiyo naomba matokeo ya tafiti zao ni batili mpaka pale watakapoamua kufanya tafiti zao kwa kuweka mazingira nadharia (Artifical Environment) kama ya uchaguzi.

Unajua unapoenda kumhoji mtu nyumbani kwake na hasa wasiojua utafiti mara nyingi wanakua waoga, Kwa maana hiyo utafiti wa Redet na Sysnovate una makosa makubwa sana ya kifundi kama ifuatavyo

Upigaji kura haufanywi kwa makarani wa kusimamia kura kufuata watu manyumbani kwao

Pia kura hazihusishi kumhoji mtu moja kwa moja au ana kwa ana

Haukua na mazingira ya Siri kama ilivyo kwenye kupiga kura

Utafiti huo huo wangepewa watu kwa siri bila kujulikana nani katoa maoni basi wangepata matokeo tofauti.
 
hata wangefanyaje mwaka huu JK kushinda ni ndoto..kaanza kuropoka huko songea eti oooh nchi itamwaga damu..hahaaaaa ..zoea tu mbona hata Moi ,Kaunda ilikuwa hivo hivo.utazoea tu mambo ya kufanya yapo mengi mbona hata kuimba unaweza kipaji unacho mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…