Matokeo ya utafiti wa kura za maoni uliotolewa juzi na REDET(Research and Education on Democracy) kuwa CCM watashinda kwa 71.2% wakifuatiwa na CHADEMA 12.3%,CUF 10.3% yanadhihirisha kuwa CCM wanawatumia REDET kuwashawishi Watanzania kuwa bado wana kubalika waktiukweli wenyewe hauko hivyo.
Matokeo haya yamekuja wakti bado watu wanatafakari yale matokeo ya kura za maoni yaliyotolewa na Synovate ambao nao wanatuhumiwa kwa kuchakachua matokeo halisi ya kura za maoni ili kui-favour CCM baada ya Synovate kukumbana na ukweli halisi wapinzani wakiongozwa na CHADEMA ndo wanongozae kwenye maoni ya uchaguzi wa Urais kwa mwaka huu wa 2010!
Hii imedhihirisha kwamba matokeo haya ya kura za maoni(poll opinions) ni ya kugushi ili kuwafurahishi CCM na kuwaweka kwenye nafasi ya ushindi baada ya 31 Oktoba. Kwamba CCM watafanya kila mbinu kupindisha matokeo ya uchaguzi ili wapinzani wakilalamika REDET na Synovate watumike kama cover ya kuficha wizi wa kura!!!
Maoni ya REDET na Synovate ndiyo yakayotumiwa kama kigezo na JWTZ kuwadhibiti wapinzani kuwa LAZIMA WAKUBALIANE NA MATOKEO KWA SABABU REDET NA SYNOVATE walitangaza hivyo hata kabla ya Uchaguzi.
Hii ndiyo janja ya CCM kwa mwaka huu wa kutumia taasisi hizi kama kigezo cha kuwa-fool Watanzania kuwa pamoja na ukweli kwamba Wapinzani wanaonekana kukubalika kwenye Kampeni zao bado chaguo la watu ni JK na CCM.
If you think critically about these opinion polls utaona kwamba hawa jamaa wa Redet na Synovate wamefanya utafiti wao kwenye maeneo ambayo ni ngome za CCM. Kwa maana ya kwamba waliowahoji katika kutoa maoni yao aidha ni viongozi wa CCM au Wanachama /Wakereketwa wa CCM. Unapofanya Research huwezi ku-base kwenye eneo moja lenye ushabiki wa kitu unachokifanyia utafiti. Lazima ufanye random research kwa watu wa aina zote wenye sifa za kupiga kura.
Naamini kabisa hawa jamaa leo hii na hasa Redet wakiambiwa watoe orodha ya aina ya watu waliowafanyia mahojiano watakuwa ni wale wale wana-CCM kwa maana ya Makada,Viongozi na Wanachama wa CCM. Kama umepanga kuhoji watu 10 ili upate maoni yao kuhusu Uchaguzi wa mwaka huu, na ukaenda eneo la CCM kwa maana ya Kiongozi wa Kitongoji au Balozi lazima kaya 7 zitasema CCM wanafaa. Hii ni asilimia 70 kwa mahesabu ya chapchap.
Naamini kama Redet naamini kama
wangelifanya utafiti wao hapo Chuo Kikuu wanafuzni wakiwepo wasingepata hiyo 71.2%
Benson Bana na Mukandara wameshinikiza UDSM isifunguliwe ili waweze kutengeneza mazingira ya ushindi wa kishiindo wa Chama Twawala-CCM.
Na hii yote ni kutaka kujikomba kwa Kikwete ili atakapoingia Ikulu awakumbuke katika ufalme wake kama ilivyokuwa kwa Prof. Beno Ndullu ambaye kwa sasa hivi ndiye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.
Ni aibu kwa wasomi mahiri kama Prof.Mukandara na Benson Bana( Bunsen Burner) kuudanganya umma wa Watanzania kwa maslahi yao binafsi na CCM.
Mimi nataka niwakumbushe kile alichokisema Msajili wa vyama Mhe.John Tendwa kuwa WAPINZANI MWAKA HUU WANAWEZA WAKASHINDI VITI 80 VYA UBUNGE AU ZAIDI YA HAPO WAKIJIPANGA VIZURI.
Kwenye Bunge lenye jumla ya viti 250 vya Ubunge viti 80+ si ushindi mdogo. Hii kwa hesabu za haraka haraka ni zaidi ya asilimia 32+.
Lakini hebu tusubiri hiyo tarehe 31 Oktoba,2010 tuone nani msema kweli kwa sharti kwamba CCM wadhibitiwe wasije iba na kughushi matokeo.
Slogan ya Leo: TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA. Chagua SLAA,CHAGUA CHADEMA. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.Ameeeen!
.