Myahudi Jr II
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 6,816
- 8,809
Habari wana Jamii Forums,
Leo napenda kuwashirikisha ndugu zangu ninyi mambo kadha wa kadha juu ya uhamiaji.
Najua Tanzania tuna watu wengi sana wanapenda kufanya kazi nje, pia ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu, na pia hata walioajiriwa bado hawana tofauti na wasiyo na ajira (wao pia hulalamika maisha magumu). Afadhali yao na wasiyoajiriwa ni moja tu wameridhika.
Tanzania ukitaka ufurahie maisha na ajira hakikisha unakua 'single', usiwe na mtoto, wala usiwe na wanaokutegemea, yaani pesa yako ni wewe tu. Hakika utafurahia kidogo ulambishwacho.
Canada wameongeza orodha ya kuhitaji nguvu kazi katika nchi yao, ni kweli wanahitaji, Watanzania tuchangamke ndugu zanguni, Wahindi wanatumia hizi fursa sana. Sasa hivi wnaruhusiwa kujiunga na Jeshi kwa walio na ukazi wa kudumu na hata Kingereza ni tatizo ila wanatoboa.
Ukifika hapa nakuhakikishia baada ya miaka 4 toka umefika tu wewe siyo huyo, yaani nyumbani utarudi kutalii tu, mfano ($ in CAD)
Hivi mtu una GPA ya 3.5+ unalia Tanzania,wakati wewe ni lulu kwa jirani?!
Unatakiwa vitu wiwili 2 tu;
1) Nenda British Counsil pale kafanye IELTS score band 7+ hakikisha unajiandaa kweli, usiende kupoteza 700,000 yako,
2) Unatakiwa uwe na “Educational credential assessment (ECA)” hii ni kama TZS 550,000 ndani ya miezi 5 unakua tayari kwa kuomba “Ukazi wa kudumu”.
Watakuja wazee wanaochaji watu TZS 10,000,000 kuwaombea kusema nimekurupuka, bado kuna vitu vingi. Hivyo vitu vingi kikubwa ni pesa ya kuonesha unaweza kuishi mwaka mmoja ambacho wanataka CAD 12,000 sawa na TSH 17,000,000.00, uoneshe benki (kwa mfanya kazi wa serikali unakopa unaweka bank, kuna wazazi wana pesa wanaweza kuwapa watoto wao), wengineo anzeni na hivyo vya juu kwanza kuna njia za wahindi wanatumia, nitawaeleza wakati mwingine.
Watakuja tena watu ukiwa na hiyo pesa si bora ubaki bongo, utatoboa, Bongo kutoboa mpaka uibe na rushwa
Siku ukiwa na IELTS 7band nitakuelekeza jinsi ya kuomba LCA, ambayo ni wewe, chuo na Ubalozi wa Canada. Malipo unalipia kwa kadi, wala usije hangaika lipa mamilioni kufanyiwa wakati ni vitu rahisi.

- Daktari analia hana ajira na mshara hautoshi.
- Injinia nao wanalia.
- Manesi na wakunga wanalia.
- Wachumi nao wanalia n.k.
Canada wameongeza orodha ya kuhitaji nguvu kazi katika nchi yao, ni kweli wanahitaji, Watanzania tuchangamke ndugu zanguni, Wahindi wanatumia hizi fursa sana. Sasa hivi wnaruhusiwa kujiunga na Jeshi kwa walio na ukazi wa kudumu na hata Kingereza ni tatizo ila wanatoboa.
Ukifika hapa nakuhakikishia baada ya miaka 4 toka umefika tu wewe siyo huyo, yaani nyumbani utarudi kutalii tu, mfano ($ in CAD)
- Mshahara wa daktari kwa mwaka (general doctor) ni $260,000.00.
- Mfamasia $90,000 kwa mwaka.
- Nesi $75,000 kwa mwaka.
- Injinia $109,000 CAD.
- Mwalimu $70,000.
- Dereva wa lori $45,000 kwa mwaka.
- Fundi seremala $43,100 CAD kwa mwaka.
- Mmwaga zege $45,187.
- Mpiga rangi $38,400.
- Kibarua wa ujenzi $38,026.
- IT $100,000.
- $6,997 kwa mwaka($583.08 per month) kwa kila mtoto anayestahiki chini ya miaka 6.
- $5,903 kwa mwaka ($491.91 per month) kwa kila mtoto anayestahiki mwenye miaka 6 mpaka 17.