Canada yahitaji zaidi watu (soma)

Canada yahitaji zaidi watu (soma)

Habari wana Jamii Forum….



Leo napenda kushare na ndugu zangu nyinyi mambo kadha wa kadha juu ya uhamiaji,

Najua Tanzania tuna watu wengi sana wanapenda kufanya kazi nje, pia ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu, na pia hata walioajiriwa bado hawana tofauti na wasio na ajira(wao pia hulalamika Maisha magumu) afadhali yao na wasio ajiriwa ni moja tu WAMERIDHIKA.

Tanzania ukitaka uenjoy Maisha na ajira hakikisha unakua “single”, usiwe na mtoto, wala usiwe na wanaokutegemea yaani pesa yako ni wewe tu, HAKIKA utafurahia kidogo ulambishwacho.
  • Daktari analia hana ajira na mshara hautoshi
  • Engineer nao wanalia
  • Manesi na wakunga wanalia
  • Wachumi nao wanalia etc etc
Ndugu zangu tuchangamkieni fursa za uhamiaji (INFORMATION IS A POWER) ninayoandika hapa jitahidi ufanye mwenyewe kama utaweza.

CANADA wameongeza “list” ya kuhitaji nguvu kazi katika nchi yao, ni kweli wanahitaji, Watanzania tuchangamke ndugu zanguni, Wahindi wanatumia hizi fursa sana sasa hivi wnaruhusiwa kujiunga na Jeshi kwa walio na Ukazi wa kudumu na hata kingereza ni tatizo ila wanatoboa
View attachment 2419005
View attachment 2419006

Ukifika hapa NAKUHAKIKISHIA baada ya miaka 4 toka umefika tu wewe sio huyo, yaani nyumbani utarudi kutalii tu, mfn ($ in CAD)
  • mshahara wa Dotka kwa mwaka (general doctor) ni $260,000.00
  • Mfamasia $90,000 per year.
  • Nurse $75,000 per year.
  • Engineer $109,000 CAD
  • Teacher $70,000
  • Truck driver $45,000 per year
  • Carpenter $43,100 CAD per year.
  • Mmwaga zege $45,187
  • Mpiga rangi $38,400
  • Kibarua wa ujenzi $38,026
  • IT $100,000
Hapa kuna child support ni
  • $6,997 per year ($583.08 per month) for each eligible child under the age of 6
  • $5,903 per year ($491.91 per month) for each eligible child aged 6 to 17
Hapo huduma za kijamii zote ni uhakika kwa 100%, kwa hapa swala la afya ni changamoto kidogo, Madaktari ni wachache kuliko watu, kwa afya 60%, unaweza Kwenda kumuona daktari saa 3 asubuhi ukatoka saa 10 jioni, hadi umeenda kwa daktari wewe unaumwa kweli, wengi naona huwa wanaenda kutibiwa kwao au wengi wanaenda DUBAI.

Hivi mtu una GPA ya 3.5+ unalia Tanzania,wakati wewe ni lulu kwa Jirani.

Unatakiwa vitu wiwili 2 tu, 1. Nenda British counsil pale kafanye IELTS score band 7+ hakikisha unajiandaa kweli, usiende kupoteza 700,000 yako, Pili unatakiwa uwe na “Educational credential assessment (ECA)” hii ni kama TZS 550,000 ndani ya miezi 5 unakua tayari kwa kuomba “Ukazi wa kudumu”

Watakuja wazee wanaochaji watu TZS 10,000,000 kuwaombea kusema nimekurupuka, bado kuna vitu vingi, hivo vitu vingi kikubwa ni Pesa ya kuonyesha unaweza kuishi mwaka mmoja ambacho wanataka CAD 12,000 sawa na TSH 17,000,000.00 uonyeshe bank (kwa mfanya kazi wa serikali unakopa unaweka bank, kuna wazazi wana pesa wanaweza kuwapa Watoto wao), wengineo anzeni na hivyo vya juu kwanza kuna njia za wahindi wanatumia, nitawaeleza wakati mwingine.

Watakuja tena watu ukiwa na hiyo pesa si bora ubaki bongo, utatoboa, BONGO KUTOBOA MPAKA UIBE na RUSHWA

Siku ukiwa na IELTS 7band nitakuelekeza jinsi ya kuomba LCA, ambayo ni wewe, chuo na Ubalozi wa Canada, malipo unalipoa kwa kadi wala USIJE HANGAIKA LIPA MAMILIONI KUFANYIWA wakati ni vitu rahisi.
Unachoongea nikweli mm nimmoja wawatu nimeshajaribu iyo njia issue inakuja visa wanachelewa kutoa sanaa.kwasasa wana dili na ukrain waamiaji, student na watu wanoenda kutibiwa. Unafanya application ya visa inagonga 6mnth ircc.inaitaji moyo kwakweli
 
Sasa kila mtu akitumia akili ya we have one life ina maana Nyerere angeamua si angekula zake bata akawaachia mashimo tu.

Acheni ubinafsi jamaa, hichi kirusi kinakula taifa na kitatumaliza.
Kila sekta ina wateule mkuu hatuwez kufanana,hatuwez kuwa na mtazamo mmoja kwny maisha kila mtu yuko na goals zake
 
Kuna ukomo wa umri?

Maana michongo kama hii mara nyingi huwa na age limitations...
 
kama hizo nafasi zingekuwa zinapatikana kirahisi mbona wabongo wangeisha woote mtaani, tatizo kuna figisu sana hadi kuweza kutoboa maana hata sie wabeba boksi mpaka tunavuka tunafika pande hizi ni majaliwa kama yule wa lake victoria , maana ukiangalia hayo mavizingiti tuliyovuka ni Mungu mwenyewe anajua. watu kimsingi ni mtaji mkubwa sana ni kwa vile basi tu.
 
brother Tanzania haitakuja kuwa nchi inayoeleweka kwasababu misingi yake ilishaharibika toka mwingi ameingia madarakani
Magufuli aliweza kuibadilisha hii nchi kutoka kwenye mfumo fulani na kuwa kwenye mfumo aliotaka yeye
Mpaka leo nchi inaendeshwa kwa kuiga vitu kadhaa kutoka kwa magufuli
Umimi ndiyo ulimuangusha

Akipatikana mtu smart kama rais wa kenya alafu awe hana tamaa ya mali awe kwa niaba ya nchi na wananchi
Tanzania itabadilika yani awe ccm lakini awasaliti wenzie watu wenye akili watamuunga mkono nchi itabadilika
 
kama hizo nafasi zingekuwa zinapatikana kirahisi mbona wabongo wangeisha woote mtaani, tatizo kuna figisu sana hadi kuweza kutoboa maana hata sie wabeba boksi mpaka tunavuka tunafika pande hizi ni majaliwa kama yule wa lake victoria , maana ukiangalia hayo mavizingiti tuliyovuka ni Mungu mwenyewe anajua. watu kimsingi ni mtaji mkubwa sana ni kwa vile basi tu.
Upo nchi gani brother..??
 
Wacanada sio wajinga hawawezi kuchukua mapoyoyo kutoka Tz,mkaaribu kizazi Chao,watu hata kudai haki zenu za msingi mnaogopa kaeni kwenu mnywe maji ya kisima

Ndio Tanzania yetu, siku kikinuka mtaona wanaisasa na watoto wao wanavokimizana JK Nyerere, kila mwanasiasa anahakikisha mwanawe ana uraia wa nchi zenye maisha mazuri, mtu una degree unakuaje poyoyo
 
Vigezo wanavyo taka ni mtihani kwa wahitaji wengi achilia mbali passport! Kwa gharama hizo wanahitaji matajiri wakafanye kazi

Kama Passport ya 150,000 ni ngumu kupata hata kwa miezi 6 ndugu yangu basi usiombe, hivi wengine wanawezaje, kuna nchi in awatu masikini kama India? mbona wanaweza
 
Kuna ukomo wa umri?

Maana michongo kama hii mara nyingi huwa na age limitations...

Ndugu haina umri, Kama una watoto na unataka watoto wako wapate elimu, malazi, maisha basi waondoe kwenye shamba la bibi ambalo wakulima wake wanaishi maisha ya shida na magumu ili wanunuzi wanufaike kisha wanaanza kuwatukana wakulima.
 
Back
Top Bottom