Hivi NATO nayo itadumu kweli?!
Mi binafsi nataka Idumu kwa Ulaya, ila Marekani wamuache apigane vita vyake mwenyewe. USA ndiyo inaongoza kuwa na migogoro mingi, na imekuwa ikiwategemea nchi marafiki kumsaidia kupigana vita vyake, hivyo itapunguza fujo akiwa pekeyake na pili itazifanya nchi wanachama kufikiri kujitegemea zaidi kuliko hivi sasa kila kitu wamekuwa wakimtegemea USA.
Vita ya Iraq Marekani ilishirikisha mataifa mengi yeye akiwa kiongozi, lakini nchi marafiki walilazimika kutoa askari kwenda Iraq, na akashinda yeye lakini walipigana wengi.
Sasa kwa kelele za sasa Marekani ingeondolewa kila sehemu, na hata UN ihamishwe kutoka Marekani ipelekwe Bara jingine, na nchi wanachama wachange, tuache utegemezi kwa USA.
Angalia OAU/AU kule Adis Ababa, hawachangi hawakutani hawafanyi chochote kwasababu hakuna pesa, wanataka Marekani na Ulaya ndio watoe pesa wakutane nchi wananchama wa AU.
Kuna mgogoro mdoogo mashariki ya Kongo, wanakimbia kimbia tu, Juzi walikuwa hapa kwenye mkutano wa Pan African Energy Summit, wakakutana kwa dharura baada ya mkutono wao kujadili usalama wa Kongo, badala wamalize wakasema wakutane kama SADC uliwaona juzi Zimbabwe, Jana tumesikia tena Tanzania itaongoza mkutano wa SADC kujadili mgogoro wa mashariki ya Kongo.Tatizo nini, kama ni gharama watumie Zoom au Microsoft Team au njia zingine, kama hizo.
Kama nchi wananchama hawatoi michango, wanataka Taasisis ziendeshwe kwa pesa za nani?
SADC wanahaha, umeona wanakimbia kimbia tu kila nchi haitaki kuandaa mkutano wanakwepa gharama.
Ni vizuri Trump kapiga pin wajitegemee, tutaumia wananchi lakini ndio gharama za maisha zilivyo.