Cancer(saratani)

Cancer(saratani)

Mkuu umeongea kweli hata mie nimeishakutana nao saana hawa watu mitaani.
Wao wamepewa kazi ya kuuza tu na elimu hawana juu ya walitendalo.
Huwa nashangaa hawapo serious kabisa wakizingatia wanadeal na afya ya binadamu moja kwa moja.
Kingine hizi bidhaa zao ni za msimu tu baada ya muda hupotea na kuja product nyingine kwa jina jingine.
Wananchi wajiangalie saana kwenye haya mambo wasichukulie kirahisi rahisi tu.
Mtu wa maana ni yule anaekuelekeza aina ya chakula unachotakiwa kula na sio hizo dawa/food supplement zao.

Usiwe miongoni mwa wanaosikia tu sababu utakuwa hujafanya research na kama huna reseacrh huna haki ya kuongea. Njoo kwa ofisi uweze kuelimishwa zaidi ili uweze kuelewa ni jambo gani hili tofauti na fikra duni ulizo nazo. 0776491294
 
Come to my office as others. The point is to help others and 'm not searching for customers.

Ndugu, is this your definition of "help"??...kweli?? yaani kuja in the Forum kutangaza bidhaa na kuweka contacts??..
Sionekani katika forum kwa muda sasa lakini believe kuna watu hapa wanajua 'KUSAIDIA'..yaani ushauri mzuri, kuelekeza watu sehemu za vipimo bora, matibabu n k bila hata Consultation fee.

Hao ndio wanaosaidia.Labda nitumie lugha ya kiswahili ndugu...hakuna sehemu duniani unaweza kuweka bidhaa na gharama halafu unapoombwa kutoa maelezo juu ya kile kile ulichokisema unakimbia, na kutoa majibu mepesi(YASIYO NA MSINGI).

Jifunze kusoma, na kujibu maswali kwa UFASAHA, si lazima ujue kila kitu, lakini utaheshimika iwapo utatafuta kufahamu zaidi na kukubali ulipo na upungufu/mapungufu, mkuu.

Saratani, haitibiwi kimchezo mchezo kama usemavyo na ndiyo maana nikakueleza eleza mechanism of action ya hiyo dawa yako, katika baadhi ya saratani nilizokwisha kutaja.

Pili, Hypothetically speaking...hata kama ingekuwa inatibu, ungeeleza ni kwa kiasi gani yaani dosage mtu anapaswa kutumia hadi kupona, KUMBUKA SARATANI hutibiwa kutokana na stage of disease!

Tatu,Kuna mdau akisema eleza mahali ulipo ufuatwe kwa hayo 'maelezo yako cheap' lakini imekuwa ngumu kufanya hivyo.


The bottom line is HAKIKISHA unajizatiti kielimu, maarifa n.k kabla ya kuleta matangazo ya "dawa" katika forum.Achana na mambo ya copy and paste information.

Anyway, it's educational forum tusifanye majibizano.
 
Ndugu mwenye huu uzi achana kujibizana na watu wasioelewa wanakupotezea muda wako. Wengine wanaoelewa wanaweza kukupigia simu wakihitaji kuelekezwa zaidi hadi ulipo.
 
Usiwe miongoni mwa wanaosikia tu sababu utakuwa hujafanya research na kama huna reseacrh huna haki ya kuongea. Njoo kwa ofisi uweze kuelimishwa zaidi ili uweze kuelewa ni jambo gani hili tofauti na fikra duni ulizo nazo. 0776491294

Mkuu majibu yako ni yaleyale ya wanaouza hizi dawa mtaani na maofisini hujieleza kama wewe kwa kukariri tu ila ukiuliza kiundani hakuna la maana zaidi ya kukuambia uende ofisini kwa maelezo zaidi!!
Jipangeni sio kukurupuka tu..
Mnazungumzia suala nyeti saana kirahisirahisi tu nendeni zenu huko.
 
Mjinga huwa hata akipewa elimu anakuwa hana uwezo wa kung'amua. Yeyote mwenye kupenda kuelewa kuhusu na maswali hayo unayouliza njoo ofisini kama wanavyokuja wengine. 0776491294

Sasa umepost humu ili iweje,kama kila swali kuhusu "dawa" zako jibu ni "njoo ofisini"?
Unanikumbusha akina GNLD na Forever Life.
Dawa zinaweza kuwa nzuri ila mnaopewa kuzisambaza lazima muwe na maelezo ya kujitosheleza!
Huwezi kutuambia dawa inatibu Cancer zote,halafu tukukubalie kirahisi rahisi tu!
Medicine are specific,sasa hiyo dawa ya kutibu kansa ya ngozi,kansa ya kizazi,kansa ya damu nk ni kutupeleka kule kule kwenye utapeli wa kikombe cha babu!
Come on with relevant explanation please!
 
Nipo pamoja na wale wenye uelewa zaidi. Nashukuru kwa walionipigia na kuweza kuonana nao pia. Wenye uhitaji wa kuelewa vizuri kuhusu hii elimu ya namna unavyoweza kujikinga na cancer na namna utakavyoweza kuzuia cancer mwilini mnazidi kukaribishwa
 
Back
Top Bottom