Cannavaro astaafu rasmi timu ya Taifa, Kujikita na Yanga

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986


“NINAFIKIRI miaka 10 niliyoitumikia timu ya Taifa Stars inatosha kiukweli na huu ni muda wangu sahihi wa mimi kustaafu kuichezea timu hiyo.

“Acha niwaachie vijana wengine wanaochipukia waje kuichezea Stars kwa mafanikio makubwa katika kuhakikisha inapata mafanikio katika siku za baadaye.

“Naamini ni maamuzi sahihi kwa wakati sahihi kwangu kutangaza kustaafu kuichezea Stars, ninaamini wapo wachezaji wengi wanaochipukia watakaonirithi mimi na wakongwe wenzangu,” hizo ni kauli za beki mkongwe wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Cannavaro ambaye alikuwa nahodha wa Taifa Stars kwa miaka kadhaa, amechukua uamuzi huo ikiwa ni siku chache baada ya kuvuliwa unahodha wa kikosi hicho, ambapo cheo hicho kimekabidhiwa kwa Mbwana Samatta anayetarajiwa kutimkia Ubelgiji kwenda kuichezea Klabu ya Genk ya nchini humo akitokea TP Mazembe ya DR Congo.

Katika mahojiano maalum na Cannavaro jijini Dar es Salaam, juzi. Mambo yalikuwa hivi;

Sababu ya kustaafu
“Maneno-maneno naona yamekuwa mengi sana nikiwa naichezea Stars, yalianza mara baada ya mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Algeria kule kwao.

“Katika mechi hiyo tulifungwa mabao 7-0, kama unakumbuka mechi hiyo muda mwingi tulicheza pungufu baada ya Mudathiri (Yahya) kutolewa kwa kadi nyekundu.

“Kiukweli tulipambana kuhakikisha tunawatoa Algeria lakini ikashindikana, cha ajabu mara baada ya mechi hiyo nilionekana mimi pekee ndiye niliyefungisha, sikujisikia vizuri kwa sababu nilipambana kwa ajili ya taifa langu na mwisho wa siku naonekana si lolote.

Ehee! Amechokwa kumbe
“Kutokana na minong’ono hiyo iliyokuwa inazungumzwa huku wakitaja umri wangu kuwa ni tatizo wakidai nimezeeka, nikaanza kufikiria kuwa inatosha. Nikaanza kupata maoni kuwa niwaachie vijana wenye umri mdogo waendelee kuichezea Stars.

Sakata la kuvuliwa unahodha
“Sing’ang’anii na wala silazimishi kuwa nahodha, kikubwa ninachotaka ni kupewa heshima yangu kwanza kama shujaa niliyeipeperusha vema bendera ya Tanzania kwa mafanikio hayohayo madogo.

“Kiukweli nimepokonywa unahodha bila ya heshima, ninajisikia vibaya kupokonywa unahodha kwa kupitia vyombo vya habari kitu ambacho siyo sahihi, hali hiyo imeshusha heshima yangu kwa kiwango kikubwa.

“Nilitakiwa kupewa taarifa kwa maana ya kupewa barua ya kiofisi na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) na baada ya hapo ingetangazwa kwenye vyombo vya habari, lakini siyo kama hivi ilivyofanyika, mimi nilipata taarifa za kuondolewa unahodha na kupewa Samatta kupitia televisheni kitu ambacho siyo sahihi.

“Nilishangaa utaratibu huo uliotumika, baada ya kupata taarifa hiyo kupitia televisheni, siku iliyofuata ndipo Kocha Mkwasa (Boniface) akanipigia simu na kuniambia kuwa wamempa unahodha Samatta, nikamuitikia tu na kukaa kimya.

“Hivi alivyoondolewa unahodha Maxime (Mecky), Swed (Salum) na Nsajigwa (Shadrack) ni sawa na mimi nilivyoondolewa unahodha? Nimeumia sana, heshima yangu ipo wapi hapo sasa? Licha ya kulitumikia taifa langu kwa nguvu na moyo mmoja, leo naonekana si lolote.

Barua ya kustaafu kupelekwa TFF
“Nimepanga kupeleka barua TFF ya kuwapa taarifa ya kustaafu kwangu kuichezea timu ya taifa, kwa sababu hali inaonyesha kabisa nimechokwa, hivyo acha nijiondoe mwenyewe kabla ya kufukuzwa. Sitaki nistaafu kuichezea Stars kwa dharau kama iliyotokea ya kupokonywa unahodha bila ya kupewa taarifa.


Abaki na Yanga yake
“Nguvu zangu zote nitazihamishia katika klabu yangu ya Yanga. Hivi sasa nimepona majeraha ya enka niliyoyapata nikiwa naitumikia Stars tulipocheza na Algeria, hivyo ninaamini baada ya wiki mbili nitarejea uwanjani,” anahitimisha Cannavaro.
 
Last edited by a moderator:
Kisa eti Samata kachukua uchezaji bora wa africa kwa wachezaji wa.ndani basi anapewa unaodha hii sio sahihi ata mi nilishamgaa mkwasa kusema eti ili kumpa heshima tumeona bora apewe unahodha…!! Mess kachukua uchezaji bora mara 5 ila ukapteni katika klabu yale kaupata lini? Xavi alichukua unaodha kisa alichukua uchezaj bora? Sio kweli tuangalie soka lawenzetu linaendaje, tulinde vipaji vyetu, heshima za pekee kwakoNadir umelipigania Taifa, sifa zako zilivuma ila sisi ndio watanzania tunaofanya vitu kwa kukurupuka… huko Algelia ile mechi tunafungwa 7 Samata alionekana mara 4 tu uwanjani ndani ya dakika 90 afadhali ata ya Ulimwengu nikimuona lakini kama lawama unatupiwa wewe ilihali beki pekeehawezi fanya kitu ikiwa kiungo na washambuliaji hawakai na.mipira wanategemea nini?
 
AONDOKE NI WAKATI SAHIHI ANASEMAJE AMEPIGANIA TAIFA WAKATI GOLI SABA ZILIMPITA PALE PALE ANAZIANGALIA,TUNATAKA VIJANA SASA
 
Uswahil umekuzid ww umejawa na chuki tuuu.... samata anastahil hko kitambaaa kwanza itawapa moyo vijana wengne kupanban wafikie pale alpo
 
inasikitisha sana ..huyu mkwasa afukuzwe hapo taifa stars yeye ndie alitufungisha magoli saba algeria...hana lolote level yake ni Twiga stars.
 
Namsapoti Nadir Haroub Cannavaro asilimia mia. Wamemkosea heshima kwa kumvua unahodha bila ya sababu yeyote, wakampa mwingine kwa upendeleo tu. kistaarabu hata kama waliona Samatta anafaa kuwa nahodha wangesubiri siku kambi ya stars ikiwekwa ndio wafanye uamuzi kama huo. Soka la bongo balaa
 
samatta ana uzoefu gani mpaka apewe unahodha? Mbona alivyokuwa tp mazembe hakupewa huo unahodha?
 
ALIYEKWAMBIA UZOEFU NDIYO KIGEZO NI NANI?lazma uangalie nahodha ana impact gani kwa wenzie,tatizo sio nani alifanya nini ila ni wakati wa vijana huu
Kwan Samata alifanya nini katika ile mechi?
 
bravo canavaro, umetumikia taifa kwa moyo mmoja, ila wapenda sifa za kijinga ndo wameona wakimpa C hyo ndo wamemthamini sana kumbe wanaua soka kwa unafiki wao, bhasi na ulimwengu wampe unaodha msaidizi maana yeye pia amechukua Africa champions league kuliko uyo boko ambae ni bure tu katika national team, tutegemeee week zingine kwenye mashindano
 
Mimi nakubaliana na Cannavaro. Huyu Mkwasa anakuwa kama mtu aliyekurupushwa kutoka wapi sijui.
Amemvunjia heshima Cannavaro.

Ila siungi mkono Cannavaro kustaafu mpira kwa sababu tu ya kupokonywa unahodha. Acheze angalau mwaka mmoja ili warithi wake ambao nahisi watakuwa bora zaidi, Salim Mbonde na Abdi Banda wapevuke zaidi na kuwa tayari kuziba pengo lake
 
Namuunga mkono, mwenyewe sikufurahishwa na kuvuliwa kwwke unahodha, eti kisa kuna mtu kachukua tuzo ya mchezaj bora wa ndani Africa.
 
unamshangaa mkwasa kukutoa unahodha kupitia simu? usisahau ni mkwasa pia hakupiga kura za FIFA kwa mchezaji bora sababu alikosa internet aaaah aaah
 
Anacholalamika Nadir sio kupewa samatta ucaptain bali ni kwanin hakujulishwa na kocha kuwa tumeamua kufanya hili kwa ajili hii then taarifa zitolewe kwenye media lkn yy anasema amepata taarifa toka media ndio siku inayofuata kocha anampigia simu hii sisahihi kbs.
 
AONDOKE NI WAKATI SAHIHI ANASEMAJE AMEPIGANIA TAIFA WAKATI GOLI SABA ZILIMPITA PALE PALE ANAZIANGALIA,TUNATAKA VIJANA SASA
Hebu Mkuu tulijadili hili swala kwa mujibu wa jina lako: 1. Brazil walifungwa 7 - 1 nyumbani na Ujerumani kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia za mara ya mwisho. Kwa bahat nzuri nahodha wa Brazil alikuwa - kama alivyokuwa Nadir Haroub kwenye 7 - 0 za Algeria - ni nahodha Luiz Gustavo. Ndiye aliyejiuzulu, au alijiuzulu kocha Scolari? 2. Ni sahihi kitabibu, kiungwana na kisaikolojia kumuuzulu mtu cheo akiwa anauguza majeruhi, tena akiwa hana kosa lolote?
 
Mkuu Team Captain alikuwa Thiago Silver kama sikosei ila ile mechi alikuwa benchi kutokana na kadi nyekundu kama nakumbuka vizuri lakini mpaka leo hajavuliwa ucaptain na isitoshe kuvua mtu ukampteni ukampa mwingine linaweza fanyika ata anapokuja kocha mpya, ya Canavaro sawa na.leo Terry pale Chelsea umvue kirahisi tu eti kisa Hazard kisa kachukua uchezaji bora uo utakuwa uwendawazi sasa akija mwakani akichukua mwingine huyo mutamvuanae mukampa huyo wa mwakani…!! Ukapteni munafanya kama njugu banah
 
Kwa mtu mwenye weledi fulani wa mpira wetu wa kitanzania pamoja na mchango wa wachezaji wetu kwenye timu ya taifa huwezi kusahau mchango wa Canavaro kwenye timu yetu ya taifa, ukianzia enzi hizo mpaka kwa maximo mpaka hii leo. Ndiyo mbwana samata katuletea sifa kwenye nchi yetu, pamoja na sifa aliyotuletea, ndiyo apewe ukepteni glafla hivyo! na je kulikuwa na sababu gani ya kumnyang'anya ukepteni Cannavaro kwa kumdhalilisha kivile pasipo kutambua mchango wake kwenye timu yetu ya taifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…