Cannavaro astaafu rasmi timu ya Taifa, Kujikita na Yanga


kumbe hapa tatizo ni:
  • kukasirika kupokonywa unahodha.
  • na yeye kumbe alitaka kupewa kiwanja, hela na atembezwe mitaani kama mbwana samata.
  • kwanini wamemshtukiza badala ya kumuandaa ili na yeye pengine aende akaroge vizuri kwao kama kawaida yake.
  • huu uamuzi wake siyo wa kiutashi bali ni uamuzi uliotokana na hasira pamoja na gere kwa mbwana samata.
binafsi nimefurahi mno kusikia kuwa ameamua kuachia ngazi kwani sijawahi kuona nahodha wa timu ya taifa mzembe na asiyejua kucheza mpira kama nadir haroub " cannavaro " na ametugharimu sana. na hizi sababu zake zimetufanya sasa tuamini kuwa ana chuki zake tu binafsi na mbwana samata na ndiyo maana pamoja na kuwa nahodha lakini tokea mbwana samata apate ile tuzo yake yeye cannavaro kama nahodha hajathubutu hata tu kumpongeza mbwana samata hadi hii leo anaamua kutundika madaluga kwa chuki.

hata hivyo natambua kabisa kuwa nadir haroub " cannavaro " ni mcheza karate mzuri na mwenye mkanda mweusi hivyo si vibaya akiwa na yanga yake awafundishe akina donald ngoma, amis tambwe na malimi busungu kucheza karate kwani najua tayari keshawafundisha akina kelvin yondan na mwenzake mbuyu twite.

nadir haroub " cannavaro " nenda tu baba usituchoshe na unaweza sasa ukaenda kuyaendeleza hayo majungu yako huyo yanga kwako ila kwa taifa stars nahodha sasa ni mbwana samata na msaidizi wake ni john boko a.k.a ndole.
 
Tatizo la viongozi wa soka katika club zetu hapa nchini na TFF wamejaa uswahili mwingi, wazee wa zengwe, embu fikiria tuu msemaji wa timu anatakiwa kuwa mtu mwenye taaluma na weledi wa hali ya juu ila hapa bongo ni mtu anayeweza kuropoka na kuponda wapinzani au kutoa majibu ya mkato kwenye vyombo vya habari...nonsense

Suala la kumvua unahodha cannavaro TFF wampe onyo kocha, na kumuomba samahani cannavaro, endapo wachezaji wakiamua kumsusia huyo jamaa yao na kocha timu haitakuwa stable
 
Kwann Boko? Wampe Ulimwengu bas
 

wewe mtie ndimu " mlazimishe " huyo cannavaro wako kuwa aendelee kuichezea taifa stars halafu tukifungwa safari hii " tumpopoe " na mawe pale taifa. inshort hatumtaki aende zake tu! zengwe letu la kwanza limeshafanikiwa na sasa tunaingia katika zengwe la pili la kumfukuzisha pia kazi boniface mkwasa kwani tumegundua analeta " uyanga fc " wake ndani ya national team badala ya kuwa " neutral ". utamuwekaje nje kwa mfano mtu kama jonas mkude au mohamed hussein tshabalala au ramadhan kessy au isihaka hassan na kumuanzisha tu kwa muda mfupi fundi said ndemla " iniesta " wa bongo na kutuwekea michezaji ya yanga na azam iliyo mibovu? nae ataondoka tu!
 
Kumbuka team ya taifa co club, kumbuka messi ndio kapten wa team ya taifa lake na alinyang'anywa mascherano… na Ronaldo pia, kw heshima ya Samatta alistaili kabsa kupew uo ukapten, sema kilichokosew n namna walivyomvua uo ukapten haroub ndo awajamtendea haki.
 
Kuwa kampeni wa timu kwa ngazi ya klabu na taifa ni zaidi ya umaarufu ila naona kwa soka letu hasa kwa Afrika tumeshindwa kuzingatia hili.Unaweza kuwa maarufu au mchezaji bora lakini ukawa huna nidhamu au haiba ya uongozi,sasa sijui huo ukapteni wa nini!!

Samatta kuwa mchezaji bora bado sio kigezo cha kuwa kapteni wa timu, vipi kuhusu nidhamu,ushirikiano na wenzake, anaweza uongozi au? Naona Mkwassa na TFF wamemkosea sana heshima Canavaro. Ina maana mwakani Singano Messi akiwa mchezaji bora afrika,Samatta atapokonywa ukapteni? Hivi mtu kupewa heshima mpaka apewe ukapteni?

Shenzy kabisa TFF na Mkwassa, mnaua soka la Tanzania kwa akili za kijinga na kujikomba komba.
 
kwetu sisi tunataka vijana wachukue usukani kwa muda aliokuwa yeye nahodha hajafikia malengo ndio maana tunabadili upepo ili kuwapa hamasa vijana wakiona wanaongozwa na kijana mwenzao tena akiwa na ndoo ya africa wewe huoni ina hamasa hiyo mkuu,majungu peleka pemba,sio kila kitu mpaka aamue JECHA mkuu mengine tunaamua wenyewe,
 
Mijadala kama hii yenye kuongozwa na itikadi za uSimba na uYanga huwa hakuna suluhu wala tija.

Lakini ni heri maamuzi hayo kayafanya Mkwasa ambaye damu inajulikana LAITI ingekuwa kafanya KIBADENI huo moto wake sijui ungekuwaje.

Lakini kwa vyovyote kama TAARIFA zenyewe alizipata kwenye VYOMBO VYA HABARI kwa kweli wamemvunjia heshima.
 
Nakumbuka enzi za Mbrazil Maxmo kuna kapten fulani hivi alistaafu team ya taifa na akaagwa kwa mechi maalumu, kama sijakosea ni Salumu Swed au Meky kocha wa Mtibwa, sasa why na kwa Cannavaro haikufanyika hivi?!
By the way, anaondoka stars akiwa na record tamu sana ambayo hakuna mchezaji mwingine aliyewahi kuipata duniani im sure.
1.Capten wa klabu yake (Yanga)
2.Capten wa team ya taifa ya ZNZ
3.Capten wa team ya taifa Tanzania.
Hakuna mchezaji aliyewahi kuwa capten wa team tatu kwa wakati mmoja!!
Go Cannavaro go ulipo tupo!!!
 
Mkuu na kundalini na wewe Team Captain alikuwa Thiago Silver, ila kwa kumpa mlinganisho sahihi mchangiaji Msemakweli nilibidi kumtolea mfano match captain wa siku ile. Nakubaliana na hoja zako kwamba Unahodha si sadaka wala njugu kwamba kila mtu kila wakati apewe.
 
Jambo la kuwa captain wa nchi ni jambo kubwa sana na lina heshma yake namna walivyo mpoka si kiungwana walifaa wamtaarifu hayo mengine ya kustaafu siwezi kuyazungumzia coz yamekaa kama kuzila au kususa flan hivi.
 
Binafsi naona kilichofanyika sio cha kiungwana, utaratibu wa kuvuana vyeo kwanjia ya media au simu haupo katika taasisi yoyote isipokua tu kwa kuonana naye au kwa maandishi ( barua). Cannavaro anahaki kufanya hayo anayokusudia kwasababu kadharauliwa kama sio kunyanyaswa
 
Amechelewa Mno, Ilikuwa Atangaze Miaka 4 Iliyopita!! Kama Ilivyokuwa Kwa Maxime Wa Mtibwa Sugar!!
 
AONDOKE NI WAKATI SAHIHI ANASEMAJE AMEPIGANIA TAIFA WAKATI GOLI SABA ZILIMPITA PALE PALE ANAZIANGALIA,TUNATAKA VIJANA SASA
hivi we unadhani Tanzania kuna beki wa kumkaba SLIMAN na MAHREZ?
Wazungu wenyewe hawajapata mbinu za kumkaba vipi kwa Tanzania?...
basi kwa taarifa yako bila kanavaro yangefika 10.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…