Cape Verde kisiwa chenye watu wapatao 600,000 kufuzu kwenda kucheza kombe la Dunia ikishinda mechi moja ijayo

Cape Verde kisiwa chenye watu wapatao 600,000 kufuzu kwenda kucheza kombe la Dunia ikishinda mechi moja ijayo

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Carpe Verde ni kisiwa kilichopo kwenye Bahari ya Atlantiki, magharibi mwa pwani ya Afrika, likiwa ni taifa dogo lenye wakazi wapatao 600,000.

Juzi kati Cape Verde aliifunga Cameroon mabingwa wa mara tano wa fainali za mataifa huru ya Afrika goli 1-0 katika mechi ilofanyika katika mji wa kisiwa hicho wa Praia.

1757571861068.png

Timu ya taifa ya Cape Verde ambayo huitwa jina la Blue Sharks au Papa wa rangi la bahari yaongoza katika kundi D kwa pointi 4 mbele ya Cameroon na kabla ya mechi hiyo walikuwa mbele kwa pointi 1.

Tanzania rushwa rushwa rushwa Tatizo kubwa Ni ccm.

Mimi nimekimbia sana umiseta kama kunwa wadau kwenye miaka2006-2011 watakuwa wananijua vizuri Kanda ya ziwa nilikuwa si zuilki na pia nilikuqa goalkeeper mzuri mno nimeanza kudaka nikiwa la nne tu hadi namaliza form4 wale wa Nyang'hwale wananijua.

Nje na mimi kuna mwamba aliwahi kuchaguliwa kujiunga na Total Africa ya mwanza lakini aliomba mlungura akakoswa na kupaji kumfia ...sio hao tu kuna watu wanakipiga vibaya mno tatizo connection na rushwa .

Taifa lenye zaidi ya watu milioni 60 linazidiwa na watu laki6 ni maajabu
 
Nyinyi huku mko milioni 60+ mmewekeza kwenye uchawa, majungu, zengwe, fitna, uchawi, umbea, wizi, ufisadi, kuoneana, na kila aina ya ujinga!

Kufanya vizuri Kimataifa kwa vilabu vya Yanga na simba, ni ushahidi tosha serikali na TFF wanatakiwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye timu za vijana, kutafuta makocha wazuri wa kuwalea hao vijana (badala ya wahamasishaji),

kuwepo na uongozi bora na wenye maono, kujenga mahusiano na academy za nje (ikiwezekana serikali ipeleke vijana wenye vipaji kupitia bajeti inayotengwa kwenye michezo ili wakifanikiwa baadaye waje walisaidie Taifa),

serikali iruhusu uraia pacha ili iwe rahisi kupata wachezaji wenye asili ya nchi yetu na ambao hawako tayari kupoteza uraia wa nchi walizo zaliwa, nk.
 
Carpe Verde ni kisiwa kilichopo kwenye Bahari ya Atlantiki, magharibi mwa pwani ya Afrika, likiwa ni taifa dogo lenye wakazi wapatao 600,000.

Juzi kati Cape Verde aliifunga Cameroon mabingwa wa mara tano wa fainali za mataifa huru ya Afrika goli 1-0 katika mechi ilofanyika katika mji wa kiswia hichio wa Praia.

Timu ya taifa ya Cape Verde ambayo huitwa jina la Blue Sharks au Papa wa rangi la bahari yaongoza katika kundi D kwa pointi 4 mbele ya Cameroon na kabla ya mechi hiyo walikuwa mbele kwa pointi 1.

Hao wengi ni wareno mdau siwezi shangaa maisha yao yapo kule kwa sana na sio hapo kisiwani
 
Tanzania badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma sababu kila mtu yuko kwa ajili ya kumrizisha rais wa inchi lakini siyo inchi yake,ndiyo maana sasa hivi CCM ni kubwa kuliko Tanzanina
 
Cape Verde wanaujua mpira vibaya mno. Kwenye ile AFCON ya Ivory Coast niliwavulia kofia jinsi walivyozihenyesha timu kubwa kama Misri na Ghana kwa kujiamini kabisa.

Nje ya uwanja pia wanajua kupendezesha pia kwa warembo wao.

Nilishajitangaza mimi ni raia mtarajiwa wa Cape Verde.
 
hapo sasa kwenye warembo hapo bhanaaa. kaka lini tunaanza taratibu za kupata uraia wa cape verde?
 
Carpe Verde ni kisiwa kilichopo kwenye Bahari ya Atlantiki, magharibi mwa pwani ya Afrika, likiwa ni taifa dogo lenye wakazi wapatao 600,000.

Juzi kati Cape Verde aliifunga Cameroon mabingwa wa mara tano wa fainali za mataifa huru ya Afrika goli 1-0 katika mechi ilofanyika katika mji wa kisiwa hicho wa Praia.

Timu ya taifa ya Cape Verde ambayo huitwa jina la Blue Sharks au Papa wa rangi la bahari yaongoza katika kundi D kwa pointi 4 mbele ya Cameroon na kabla ya mechi hiyo walikuwa mbele kwa pointi 1.

Nyie wa kila kitu, kila goli ni goli la mama hilo kombe la dunia mtalisikia/mtaliona kwenye Azam tv tu.
 
Bibilia katika kitabu cha mithali neno la mungu linasema;

"Heri yao watu laki sita wenye akili, kuliko watu milioni sitini wasio na akili".
 
Back
Top Bottom