TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
5,077
Reaction score
2,246
TANZIA:

Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam leo saa kumi jioni.

CCM Wameandika kwenye twitter yao.


Historia Fupi ya Marehemu John Komba

Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1954 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1977 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.

Chanzo: BBC
 
Mbunge WA mbinga CCM


 
Ni kweli Komba kafariki Dunia
Twiter ya CCM
 
Mbunge wa mbinga kapten john komba amefariki muda mfupi uliopita kwa shambulio la moyo ( heart attack)

alipo pelekwa hospitali ya TMJ alikuwa tayari ameshafariki dunia. Mungu awafariji wote walioguswa na msiba huu.
 
Huwa hatupendi kushabikia mauti wala kufurahia kifo cha mtu ila malipo ya kila kitu yapo hapa hapa duniani

Mshukuru Mungu kwa kila hatua na ukumbuke cheo ni dhamana usije kukitumia vibaya,

fikiria mzee warioba yupo hai ila kapten komba katangulia mbele za haki nways RIP kaptn komba sisi sote twaja
 
ilibidi jana ahudhurie sherehe za kusimikwa kwa kamanda wa UVCCM wilaya ya nyasa bwana kasiani njowoka

hata hivyo hajahudhuria hiyo jana kwani taarifa zilisema kwa sababu ya ugonjwa . kuhusu kifo mleta mada aeleze vizuri
 
TANZIA:

Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar. Ccm wameandika kwenye twitter

Rip komba
 
Kutoka Uhuru FM kuwa mbunge wa mbinga na Kiongozi wa bandi ya music ya tot mh. Capt. John Komba amefariki dunia..

Mungu ailaze roho yakemahali pema peponi ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…