TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.

Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.

Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1977 hadi mwaka 1978.

Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.


Chanzo
: BBC
 
Kweli binadamu ni masikini hana control na uhai wake, waweza tunza uhai lkn huwezi zuia kifo. Ukitazamana alivyolala hawezi kumzuia yeyote kufanya chochote . Tuwapo hai tunakua jeuri na majigambo mengi kana kwamba tuna ubia na uhai. Tubadilike , tuthamini wengine na tusitumie nafasi zetu vibaya . Tunaona humu jinsi matendo ya ndugu yetu yanavyoanikwa ukiwa kama mwanafamilia unatamani yafutike lkn haiwezekani kwani kuna walioumizwa. Mungu awatie nguvu wanafamilia ktk wakati huu mgumu R.I.P Komba
 
Mtani Komba umekwenda kweli? Jina lako lilikuwa kubwa sana. Lilikuwa kubwa kwenye CCM kwa jitihada zako za kutusi, kusimanga na kuwasigina kwa maneno mazito mazito wapinzani wa kisiasa hasa CHADEMA. Ukavuka mipaka ukatukana mpaka wazazi, mzee Warioba ni miongoni mwao. Ulikuwa shujaa mtani katika kutusi na masimango dhidi ya wote usiowataka.

Umaarufu wako ulienda zaidi kwa wale visura. Wengine walistaajabu kwa nini uwadake visura wa namna ile. Mtani wako sina ushahidi wa hawa visura, ni habari za kusikia tu. Ila kuropoka dhidi ya wazee wenye hekima kama Warioba, hakika nilikusikia mwenyewe kweupe kwa masikio yangu. Na yale maneno yako bungeni dhidi ya CHADEMA kuwa wanasema kama wanajamba jamba, hayo nayo niliyasikia.

Umaarufu wako katika kuimba, na sauti nzuri isiyoendana na umbile lako, hakika katika hilo mimi ni shahidi.

Mtani hakika nimesikitika sana kuondoka mtani wangu muda kama huu. Nilitaka uwe hai ili ushuhudie tunavyokuangusha ubunge kule jimboni mwezi wa Oktoba. Nilitaka mtani ushuhudie tunavyokidondosha chama chako, na tukuoneshe wewe na chama chako jinsi nchi inavyotakiwa kuongozwa. Maana raha ya ushindi ni kumshinda mshindani wako akiwa mzima na mwenye afya njema na awepo ili ashuhudie ushindi wako.

Mtani umetutoka, na ndugu zangu waliopo Dar na Songea wana kazi kubwa ya kulibeba jeneza lako na kuliweka kwenye nyumba yako ya milele. Uzito wako siyo mchezo, lazima karibia kilo 200. Maana naamini ule utamaduni wetu ni lazima utafuatwa na CCM na serikali itabidi wasiuvuruge. Maiti lazima ioshe na watani zake. Chakula, mahema, kaburi, sanda na maziko ni lazima watani wasimamie na kutekeleza kikamilifu.

Mtani nikuage namna gani? Komba kwa heri, tena kwa heri ya milele. Hatujui tukuimbie wimbo gani, ziandaliwe nyimbo nyingine au tupige nyimbo zako mwenyewe!

Kwa watoto, ndugu, marafiki na wangoni wote poleni kwa msiba wa mtani Komba. Baba yenu jina lake lilikuwa kubwa, kauli yake kuwa ataingia msituni ilikuwa ndiyo kauli yake nzito ya mwisho ambayo haikueleweka. Matusi yake hatuyakumbuki leo, kejeni na masimango yake hatuyakumbuki leo, madeni yake hatuyakumbuki sisi labda hao CRDB, sisi letu ni moja tunaungana kuomboleza kifo cha mtani Komba, mimi mtani wake ambaye hatukuwahi kukaribiana wala kusogeleana katika itikadi lakini niliposikia kifo chako, moyo ulishtuka kwa mshangao mkubwa.

Poleni sana familia ya Komba. Nguvu yenu ya kustahimili msiba huu ipo mikononi mwa Bwana aliyetumba vyote maana ndiye ajuaye kila mmoja siku ya kuitwa kwake. Bwana alitoa na Bwana alitwaa, jina lake lihimidiwe.
 
TANZIA:

Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam leo saa kumi jioni.

CCM na EATV(East Africa Television) Wameandika kwenye twitter yao.


attachment.php

Binadamu tunatembea na vifo pole sana wafiwa.
 
Sikumbuki mwaka gani hasa but ilikuwa around mwaka 1992 hivi au 1993
those days nyimbo yake maarufu ilikuwa 'nambari one'

alikuwa kwenye kundi lake yuko na Mzee Majuto akiigiza
Alikuwa Mwembamba kiasi..kitambi kwa mbaali.....he was healthy..

hakuwa mbunge wala hakuwa na bajeti maalum ya kundi lake la TOT

alipoanza kupewa fungu maalum la kampeni mwaka 1995 na baadae ubunge
the rest was history.....alinenepa na kunenepa......hadi leo hii...

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
 
Hawa wafuatao pia wangesepa wakaungana na capt. Komba.
-Wapigwe tu
-Serikali 3 jeshi litachukua nchi
-Nyoka wa makengeza
-Milioni 10 za mboga
-Buffons a.k.a mtaalamu wa kunasa vibao wazee.




-
 
Sasa nani atamtungia naye mwimbo Wa maombolezo sababu kamwimbia Samora, Mwalimu, Sokoine etc May God Rest his Soul in Piece.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Haya muandishi wangu mahiri ninayekuaminia nasubiri ripoti kamili.
Au ni ule mkopo aliokopaga CRDB nasikia walikua wanamdai ml.600 alizoenda kujengea ile shule yake.

Mwenzangu itakuwa ndo izo , sasa kinamchomfanya afe kitu gani? Wakati anachukua mihela bank mbona hakufa? Nfyuu apunzike kwa amani asituchoshe apa, mie unafiki sina afe hasife vichambo anavipata kama kawa...
 
Back
Top Bottom