TANZIA Captain John Komba afariki Dunia


Tumewaona! Lililobaki ni kumpa ubunge mwanae Komba kama ilivyokuwa kwa waziri wa fedha-. Just wait and see CCM!
 
Vitabu vitakatifu vishatahadharisha kuwa kila nafsi itajiamulia mwenyewe mahali gani atapapenda kufikia wakati ikionja umauti, kama ni peponi utaamua mwenyewe na kama jehanamu pia utaamua mwenyewe ukiwa ungali hai hapa duniani, Sasa hili la kumlazimisha Mungu kwamba amlaze John Komba mahala pema peponi ni kinyume na mafundishi ya Mungu kupitia vitabu vyake vitakatifu na manabii, Komba alishaamua muda mlrefu wapi anataka afikie, Kama kila anlipopata nafasi ya kuchangia hoja bungeni yeye ni matusi tuu tena kwa watu waliomzidi umri na hadhi, Lakini pia katika lile kundi lao la ccm shughuli yao kubwa ni wizi na kuonea wanyonge, naogopa kumfundisha mungu amuweke wapi bali amuweke anapostahili
.
 

Du! sijawahi kuona msiba wa kiongozi kama huu,watu wanashangilia kama kafa jangili.
 
Nakumbuka siku moja maeneo flan tukiongea uliwahi sema, Imba, imba mpaka watu waseme eee.. ongea kwa kuimba, fanya kazi kwa kuimba, hutubia kwa kuimba, siku zote watu wakisikia wimbo wako kwanza wanapata burudani na vilevile ujumbe. I salute you..

maadam nyimbo zako ziko hai bado uko hai bro.. big up..

RIP
 
Huo utakuwa ni UNAFIKI,na unafiki ni dhambi mbaya,yaani mtu siku zote unampinga na kupinga anayoyafanya hlf leo ujilazimishe kuonesha upendo.Haifai.

read between the lines,unielewe.
 
Du! sijawahi kuona msiba wa kiongozi kama huu,watu wanashangilia kama kafa jangili.

Wakati tupo wadogo kuna wimbo tulikuwa tunaimba
IDD AMINI AKIFA MIMI.SIWEZI KULIA,NITAMTUPA KAGERA KIWE CHAKULA CHA MAMBA.
DUh komba sijui.kwake.imekaeje
 
Yanasemwa mengi binafsi natakujua ukweli zaidi.

Wengine wanasema alizidi sana uzito wake Je! Kuna anayejua alifikia Kilogramu ngapi?
Je! Yamkini hio ni sababu tosha yakupatwa na kifo?

Lakini pia kuna wengine wanadiriki kuchokonoa mambo yake ya Kifedha kuwa ni MKOPO WA BILLIONI MOJA BANK YA CRDB,Baadhi ya watoa taarifa waliokuwa karibu naye wanasema alirejesha Millioni 400 na alibakiza milioni 600.

Inaonekana kulikuwa na shinikizo la kulipa madeni yote haraka kabla ya kuanza chaguzi za ndani CCM.

Mambo ya vimwana (Capt.Komba alikuwa sio duni kwa Warembo alipatikana kirahisi na kwa wakati huku akitoa MSHIKO MNONO) pia yametajwa kuwa ndio chanzo kingine cha kuwa na Madeni mengi na makubwa hata kusababisha MAUTI KUMFIKIA.

Wabongo kwa kuongea sio haba,wengine wanasema kule kujihusisha na kundi la LOWASA huenda imewafanya wakubwa wawatumie Bank zinazomdai zimfuatilie kupita maelezo.


Wanadiriki kuingia ndani zaidi na kusema huyu bwana kwa habari za mambo ya RASIMU YA KATIBA MPYA iliyowasilishwa na kusomwa Bungeni na Mzee wetu JAJI WARIOBA imemletea LAANA badala ya BARAKA hasa hapo CAPT KOMBA aliposimama na kutakamka maneno MAKALI,MAGUMU,MAZITO,MABAYA akimtusi JAJI SINDE WARIOBA.

Mzee mwenyewe amekaribia kufa usituvurugie Nchi la sivyo nitaingia msituni,maneno hayo yalitamkwa na MAREHEMU KOMBA.

Sote tumefichwa hatujui lini huyu na yule watakufa.Kifo chake komba huenda sio kulogwa bali ni MUNGU TU AMEMPENDA ZAIDI KULIKO SISI NA KUAMUA KUMWONYESHA MWENYE KUPANGA RATIBA Nani aondoke nani abakie.Mwenye uwezo huo ni MOLA PEKE YAKE.


Inatufundisha sote tusijisahau duniani sio mahali pa kudumu siku yaja tutaondoka kila mmoja na Majira yake,Tuitumie hii FURSA YA KUISHI VIZURI.


Nimebakia najiuliza maswali Mu-Kichwa NINI KIMEMUUA CAPT KOMBA kati ya haya yote yanayosemwa???
 
Hili la laana ya Jaji Warioba kama ina tiki vile ebu ngoja nisubiri mawazo ya wengine.

Apate laana kwani Warioba ni baba yake mzazi? Kama ni hivyo basi Mnyika ana laana ya JK kwa kumuita dhaifu.Tuacheni mambo ya kudhani kifo ni kifo.
 
Wengine wanasema ni ugonjwa wa kisasa wa siku nyingi tu, mengine yote ni by the way!
 
kumchuria mwenzako kifo siku zote ni kujichuria kifo wewe mwenyewe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…