Mkuu mtu kuwa mwana usalama haimaanishi kuwa amekuwa mungu kiasi kuwa atacho panga ni razima kitakuwa pafect kwa asilimia 100.
Hili suala la kamanda Tesha hakuna anaye jua kati yako na huyo unaye mpinga bali nyote mnaongea kwa kudhania tu ambaye jua ukweli juu ya hili jambo ni Tesha mwenyewe na serikali.
Kama ni kweli kuwa tukio la Tesha lilikuwa la kupanga ,kwa mtazamo wangu ni wenda ulikuwa ni chambo ya kuwapata wasariti wasio mpenda mama ndani ya jeshi ila bahati mbaya mpango wao ukawa umeenda mbali zaidi na kuzaa matokeo ambayo hawa kuyatarajia.
kuna mistari myekundu ambayo hakuna Idara ya Usalama duniani inayothubutu kuivuka, hata katika operesheni za siri.
Hakuna Idara ya Usalama duniani inayoruhusu ofisa wa kijeshi aliyevaa gwanda kutoa kauli zinazochochea uasi, au kuhoji uhalali wa Amiri Jeshi Mkuu wake.
Captain Tesha hakutoa maoni ya kawaida, aliaminisha waandamanaji kuwa jeshi lipo nyuma yao na akawataka waingie barabarani. Usalama hauwezi kufanya wehu huo wa kuwasha moto kwenye nyumba iliyojaa madumu ya petroli ili tu kutafuta wasaliti...
Kama ingekuwa ni operesheni iliyopangwa na serikali, rais asingepoteza muda kwenda kutuliza hali ya hewa na kuomba utii wa jeshi , Kwenda kwake kulionyesha wazi uwepo wa nyufa ndani ya vyombo vya ulinzi.
Rais Alpha Conde aliamini amezungukwa na wasaliti, akaanzisha kikosi maalum cha kijeshi chini ya Kanali Doumbouya ili kulinda utawala wake na kudhibiti wapinzani. Conde aliamini anacheza karata salama ya kiusalama , matokeo yake? kikosi hicho hicho kikaja kumpindua yeye mwenyewe mnamo Septemba 2021.
Jeshini hakunaga wehu na ujinga kama huo, huwezi kuchea na moto hali ya kuwa inafahamika kabla ya Ot 29 nchi ilikuwa katika hali ipi kisiasa...
Military discipline ndio uhai wa Taifa, Huwezi kuitumia kama karata ya kamari ya kisiasa. Hakuna mastermind wa usalama mwenye akili timamu anayejua madhara ya kijeshi atakayeruhusu ofisa wa jeshi aasi mtandaoni kwa lengo la kutega watu, acheni hizo story za kwenye vijiwe vya alkasusu mujarab.
Ukweli ni kwamba serikali ilijikuta kwenye wakati mgumu kutokana na hasira za wananchi zilizosababishwa na wimbi la utekaji na uvunjaji wa haki za binadamu kabla ya MO29, na dhoruba hiyo ikazua mawimbi ndani ya jeshi yaliyomfanya Captain Tesha kuongea alichoongea. Kila kitu kilikuwa halisi... msitake kuleta hadith za kutunga...
Unasema mimi mwenyewe nadhania tu, lakini nimetoa facts, wewe hata facts huna, maana unachosema hakina facts zozote zile...