Licha ya kuanzia benchi wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza, #ManUnited imeshinda 3-0 dhidi ya Charlton Athletic, wafungaji wakiwa ni Antony na Marcus Rashford (mawili) kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Mchezo mwingine wa Robo Fainali, Newcastle United pia imesonga mbele kwa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Leicester City kwenye Uwanja wa St James' Park.
Michezo mingine ya Robo Fainali itachezwa leo Januari 11, 2023, Nottingham Forest dhidi ya Wolverhampton, Southampton na Manchester City.