Carbon credit business

serikali yetu mpaka leo hawajui biashara hii licha ya kuwa na misitu kibao, kuna baadhi ya wabunge walikuja hapa tukawaeleza wakabaki kutoa macho.........


Ndg. yangu Edson.....ulitaraji wafanye nini cha ziada.........................hawana ziada;
 
Mbarikiwe nyote wenye mapenzi mema na wanajamii wenzenu! mkuu Edson na Mkuu Malila tuko nyuma yenu !
 
Nimecheka kidogo niliposoma Edson akisema Serikali haijui chochote kuhusu Carbon Credit Business wakati Mradi wa Green Resource Mufindi ulipitishwa/Idhinishwa na Serikali. Edson Serikali kwako ni nini? Ni Wabunge tu? Tatizo la Serikali ni Urasimu wake ndiyo maana mambo yake yanakua slow kuliko Private sector. Suala la Carbon Credit siyo la leo Serikalini.
 
Nilipotea kidogo,

Nilikwenda Mafinga Grl na kuonana na mkuu Edson,ilikuwa siku nzuri kwangu,kwanza kuonana na m-jf mwenzangu,pili kuona Wenzetu wanafanya nini kwa kuunganisha nguvu. Nilionana na wanene wa Edson kwa msaada wake,kweli wako vizuri,walinisikiliza na kunipa majibu ya maswali yangu. Kwa ufupi ni kwamba; biashara hii ipo na wao Grl wanafanya na tayari wameshapata malipo, sisi wadau ambao sio makampuni ni lazima tuwe na kikundi kilichosajiliwa na kutambuliwa na serikali, tatu mashamba yetu lazima yawe na title deed. Tukikamilisha hayo basi niwaone ili niunganishwe na wahusika huko London. Kwa ufupi ukifanikiwa kuwafikia hawa jamaa ni hela nzuri sana.

Zaidi sana,niwakaribishe ktk biashara hii ya misitu. Asante sana mkuu Edson kwa msaada wako. Niliondoka pale ofisini kwenu nikiwa na usongo mpaka kieleweke.
 
Hiyo carbon inapimwa vipi?
Bei anapanga nani, Mmiliki au mnunuaji?
Vipi kama nitahitaji msitu wangu kwa kazi nyingine?
Niliwahi kuattend seminar flani wakaongelea na hii carbon trading ila sikuielewa elewa.
 
Hiyo carbon inapimwa vipi?
Bei anapanga nani, Mmiliki au mnunuaji?
Vipi kama nitahitaji msitu wangu kwa kazi nyingine?
Niliwahi kuattend seminar flani wakaongelea na hii carbon trading ila sikuielewa elewa.

Wanapima hivi, nikikosea nisamehewe. Wanachukua kipenyo cha miti yako, wanazidisha na urefu kisha wanazidisha na umri wa miti hiyo. Baada ya hesabu hizo,wanaweza kujua ni tani ngapi za hewa ya ukaa zilinyonywa na miti yako toka angani. Bei ziko na madalali wa biashara hiyo, kwa hiyo kuibiwa ni lazima. Ukiutaka msitu wako, itakuwa ndio mwisho wa mkataba wako na wao.

Kinacholeta shida ktk biashara hii ni kwamba,wanaojua nini kinafanyika kwa usahihi,wako kimya. Ukiongeza na ulegelege wa serikali yetu ndio basi tena. Offcial dealers ni wachache sana, kiasi kwamba hawana muda wa kutosha ili sisi wakulima wa vijijini tuweze kuwafikia.
 
<br />
<br />
kweli kuna kiharufu cha wizi. Ahsante.
 
Nahisi kama tunachelewa vile kadri tunavyozidi kujadili humu,
je nikipanda miti ya mbuyu au mianzi si ndio tutavuna pesa nyingi zaidi, embu tutafakari unene wa mbuyu plus urefu wake, au mianzi kwa inavyokuwa fastafasta,

anyway, Mkuu Edson ,tupe plan nzima ili tuifuate mguu kwa mguu ,tukingoja serikali hatufiki kokote kwani after 50yrs bado main roads hazina lami.hili swala its too serious kuwaachia politicians
 
HIYO MITI ITAKAYOPANDWA NI YA AINA GANI?.NI YA KIGENI AU NI YA ASILI YA HAPO UNAPOTAKA KUPANDA?.CARBON SINK PROGRAM NI PROGRAM AMBAYO INARUDISHA ARDHI YA UOTO WA ASILI WA SEHEMU HIYO.KWA MFANO INATAKIWA WAZEE AU MZEE AMBAE YUPO HAPOUNAPOTAKA KUPANDA MITI AKUAMBIA YUPO HAPO KWA MUDA GANI?KAMA AKIKUAMBIA ANA MIAKA ZAIDI YA 60.MNATAKIWA KUMWUULIZA .HAPO ZAMANI HAPA KULIKUWA NA UOTO GANI WA ASILI,MITI GANI,WADUDU GANI?.NDIPO ZOEZI LA KUPAMBANA NA GLOBAL WARMING LITAFANIKIWA.TUNARUDISHA HADHI YA MIAKA HIYO YA NYUMA.TUANGALIE TULIKOSEA NINI?.MIMI NITATOA TAA ZA SOLAR NA REDIA INAYOCHARGE SIMU YAKO NDUNGU MTANZANIA KWA ATAKAE ONYESHA ANAPANDA MITI YA ASILI KIJIOGRAFIA YA SEHEMU ILE NA IKASIMAMA NA IKAZIBISWA .
POLLUTION CONTROL AGENCY
5912 14TH STREET ,SUITE 206
NW,WASHINGTON DC
Lmhagama@yahoo.co.uk
phone 011 [1] 202 367 2761

POLLUTION CONTROL AGENCY
P.O.BOX 13031
DAR ES SALAAM
 
Wengine wan hamasisha kupanda miti wengine wana harakisha ukataji miti.kwa kuwaambia wale waliopata mashamba mapya kuwa wasipo safisha shamba watanyang'anywa.hii ni akili ya serikali ya hii nchi inayoitwa tanzania.
 

Bahati mbaya mimi nilianza na miti exortic, hii ya kiasili tatizo liko ktk umiliki, serikali inasumbua sana. Baba yangu alipanda miti ya kiasili kuzunguka nyumba yake, ni mizuri sana kwa mbao, lakini tukitaka tuvune japo mmoja ili tupate frames za milango tunasumbuliwa sana, mara vibali mara nini. Mwaka jana niliotesha miche kidogo ya miti asili karibu na shamba langu, sipendi kuendelea kwa sababu ya sera ya nchi. Mimi wakinipa kibali cha kuipanda na kuimiliki, naweza kuipanda kwa malaki kwa sababu napanda miti ya mbao kila mwaka isiyo pungua laki moja.
 

Mwaka jana nilipanda miti hiyo jamii ya mivengi michache, ni mizuri sana ktk vyanzo vya maji, tatizo ni ownership mkuu. Wakuu wa serikali wakitoa ushirikiano tunaweza kufanya kwa large scale bila taabu.
 
Kwa sababu ya umaskini, tunakubali kukumbatia kifo! carbon credit = pesa; carbon monoxide = kifo.
 
Mimi naomba kitu kimoja hapa ndugu zang watanzania tukiangalie.tufikiri sana pesa pesa .hapana.nafikiri mnaona hali inavyobadilika huko.sisi tuliongelea jinsi gani tutaweza kusaidia kuondoa carbon dioxide na pia other greenhouse gases kutoka kwenye anga yetu.mimi ni mshauri wa ngo moja kule kenya na pia hapo tanzania ni mshauri wa ngo inaitwa pollution control agency.ngo yetu ina vifaa vingi sana ,kwa ajili ya kupima carbon dioxide na tumefanya hivyo ,siku za nyuma ili kutafuta data.na nakuambieni nmc wanatujua ,ofisi ya makamu wa rais wanajua pia.sasa naomba kama kuna watu kati yetu hapa ana uchungu wa nchi yetu na yupo mbele kufanya hiyo kazi ya kupumguza carbon basi .mimi huku kuna pesa nyingi sana kwa ajili ya kazi hiyo .ila tunaitaji wafuatiliaji wa karibu wenye moyo.ngo yetu in credit kubwa ya kukubaliwa na kupata pesa.sasa nilitaka tuwe na mwalimu wa chuo kikuu mmoja au wawili .na mimi nitawapa maelezo.nimejitahidi sana lakini watu wa nyumbani wanaangalia sana maslahi ya hapo kwa hapo.tunasema tunapinga ufisaji basi tuanzie hapa sisi wenyewe.
 

Mimi ninafanya shughuli hizi kwa muda sasa,
Kama utafanikiwa kuwapata hao walimu wa chuo kikuu na mtakapotaka kuanza hiyo kazi, mimi niwekeni ktk operation department basi. Niko tayari kuchangia kile ninachoweza ktk kufanikisha azma hii nzuri.

Nasema naweza kufanya kwa sababu tayari nina timu ya vijana ambao wanaweza kazi kwa sababu wamekuwa trained tayari. Tunaweza kuanzia vitalu mpaka upandaji, tatizo litakuwa baadhi ya mbegu za miti asili. Naamini kwa kushirikiana na vituo vya Morogoro,Iringa na Lushoto tunaweza kufanikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…