Wanapima hivi, nikikosea nisamehewe. Wanachukua kipenyo cha miti yako, wanazidisha na urefu kisha wanazidisha na umri wa miti hiyo. Baada ya hesabu hizo,wanaweza kujua ni tani ngapi za hewa ya ukaa zilinyonywa na miti yako toka angani. Bei ziko na madalali wa biashara hiyo, kwa hiyo kuibiwa ni lazima. Ukiutaka msitu wako, itakuwa ndio mwisho wa mkataba wako na wao.<br />
<br />
Kinacholeta shida ktk biashara hii ni kwamba,wanaojua nini kinafanyika kwa usahihi,wako kimya. Ukiongeza na ulegelege wa serikali yetu ndio basi tena. Offcial dealers ni wachache sana, kiasi kwamba hawana muda wa kutosha ili sisi wakulima wa vijijini tuweze kuwafikia.