Carol Ndosi ni nani haswa?

Carol Ndosi ni nani haswa?

Status
Not open for further replies.
Hongera sana lakini nakushauri usiuze hili tamasha maana wenzio watapiga pesa...Naamini penye ugumu ndio kuna njia ya kutokea....

Halafu pengine hili tamasha unatakiwa uliweke kwenye Calender,liwe la kipindi fulani tuu na baada ya hapo una pumzika mpaka mwakani pengine unaweza ukalifanya la mwenzi mzima likazunguka nchi nzima....yaani kwa mwaka linakuwa ni mara moja tuu hii inaweza ikasaidia kupata hata wadhamini.

Kwangu mimi naona ukiendelea kukaza buti ipo siku litakuwa kubwa zaidi ya ufikiriavyo au zaidi ya sasa........

Yes that is the plan, tukirudi mwezi 6 ndio utaratibu tulioweka. Na tulishaanza kupunguza tangu mwaka jana. Naendelea kukaza buti kaka nashukuru kwa mawazo yako
 
Nakukubali sana sista, mdada intellectual. Unavyotupia kiafrika afrika zaidi,ndio unaniacha hoi.

Sema tatizo im too young ningekuja PM wallah! Nikionaga RT au like yako naiscreenshot kabisa.!!!
 
Carol Ndosi ni mtoto wa marehemu Meja Moses Jonas Ndosi ambaye ukiachilia mbali kuwa mwanajeshi, pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi Tanzania (KAMATA), pia aliwahi kuwania nafasi ya kugombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki 1995 ndani ya CCM lakini hakupata. Hivyo kwa kuelezea historia ya baba yake, itakuwa imeeleweka asili yake kwa kiasi flani.

You are very right kuhusu taarifa za Baba Yangu Mzazi hata hivyo mimi nimelelewa na Mama Yangu tu maisha yangu. Hata hiko kipindi cha kugombea sikuwa karibu hivyona Mzee wangu. Haina mahusiano yoyote na mawazo wala maoni yangu kuhusu uhalisia unaoendelea.
 
malengo hasa ya hiyo Nyama Choma festival ni nini?.....ni kuuza nyama tu kwa wateja?...

Kwa hilo ndio, tumejaribu kutengeneza platform inayowakutanisha wachoma nyama na wateja. Tuliaminu tungeweka na banda letu wenyewe tusingekua tunatoa nafasi sawa kwa wengine kwani inawezekana wateja wengi wangekuja kwetu. Huwa tunapika wenyewe kwenye event nyingine ya Sunday Cookout. Karibu sana
 
Yes that is the plan, tukirudi mwezi 6 ndio utaratibu tulioweka. Na tulishaanza kupunguza tangu mwaka jana. Naendelea kukaza buti kaka nashukuru kwa mawazo yako
Safi sana hii itawasaidia hata ninyi kuwa wabunifu zaidi halafu itafanya tamasha litangazike zaidi maana watu watakuwa wanayo Calender kichwani kuwa ikifika kipindi fulani ni nyama choma festival mpaka kipindi fulani na hii itafikia kipindi watu watakuwa wanalipisha tamasha lako bila hata kutangaza kuanza maana watakuwa na ratiba.
Mimi naamini umezungukwa na watu wengi wana maarifa na wana watu hutoweza kushindwa..
 
Kwa hilo ndio, tumejaribu kutengeneza platform inayowakutanisha wachoma nyama na wateja. Tuliaminu tungeweka na banda letu wenyewe tusingekua tunatoa nafasi sawa kwa wengine kwani inawezekana wateja wengi wangekuja kwetu. Huwa tunapika wenyewe kwenye event nyingine ya Sunday Cookout. Karibu sana
Naamini kuwapa wadau wengine walete majiko bado ni idea nzuri sana halafu ina kupunguzia wewe pressure sema wewe ni kuhakikisha standard za nyama na vitu vingine,sema wewe unatakiwa kuwekeza pia kwenye burudani maana hicho ndicho kinavutia wengi zaidi ukiacha nyama tuu...
Halafu kuwapa watu nafasi ya kufanya biashara ni jambo jema zaidi na ninafikiri liwe ndilo lengo lako zaidi na ukihakikisha unaleta burudani yenye A list artist hakika swala la kula hizo nyama pengine hazito tosha.....
 
You are very right kuhusu taarifa za Baba Yangu Mzazi hata hivyo mimi nimelelewa na Mama Yangu tu maisha yangu. Hata hiko kipindi cha kugombea sikuwa karibu hivyona Mzee wangu. Haina mahusiano yoyote na mawazo wala maoni yangu kuhusu uhalisia unaoendelea.
Asante sana, you're so creative Mungu azidi kuthibitika kupitia maisha yako. All in all cha kujivunia ni usmart wako na cyo ukabila wako. Keep it up
 
Dada Carol naomba nikupongeze, kweli usione kitu kimesimama kuna struggles nyingi Sana nyuma yake watu wamepitia, I'm talking of TNCF..

Anyway, nilishuhudia ile iliyofanyika pale UDSM, ilikua vizuri Sana. So what was the reason ya kuhamisha ile venue?
 
Utangazaji na uandishi wa habari ni calling yangu ya kwanza, hata niikatae vipi inarudi lol..so sijaacha, matter of fact, narudi kwenye a screen near you mwaka huu.

Na kuhusu TNCF- hapana haijafika kwa kweli level tunayotaka. Tuna mipango mingi ya kuboresha na tuko mbioni kulaunch barbecue sauce yetu wenyewe na barbecue house. Insh’allah kheri kila kitu kwa wakati, all we can do is keep pushing.
Safi sana hapo kwenye kutangaza nimefurahi zaidi...nilikuwa napenda sana siasa za siasa halafu wakati kipindi kinakuwa maarufu zaidi ndio kikakata.....
 
Dada Carol naomba nikupongeze, kweli usione kitu kimesimama kuna struggles nyingi Sana nyuma yake watu wamepitia, I'm talking of TNCF..

Anyway, nilishuhudia ile iliyofanyika pale UDSM, ilikua vizuri Sana. So what was the reason ya kuhamisha ile venue?

It was too much for the administration, walisema haiendani na academic values za chuo. Siku wanafunzi walihudhuria kwa wingi mno, mlimani peke yake kuna 30k students. Wengine walizidiwa na starehe na kusababisha usumbufu kwenye residential houses and properties. Uongozi uliona ni vyema kusitisha matumizi. But its one hell of a venue kwa kweli. Tuliweka historia pale.
 
Am excited too...Tunahitaji sana local content nchini. Deo Volente
Nini kilitokea kwenye kipindi cha siasa za siasa? Nilikipenda kweli kile kipindi.

And naomba nikuambie una customer care nzuri. Last time Nyama Choma Moshi tulikutana na wewe tukiwa tunatoka. Ukatusimamisha like mnaenda wapi mbona mapema au mmeboreka. Tukakuambia tunatoka mara moja tunarudi.

Kweli tulikuwa tumeboreka ila ukatumbia tusubirie Aslay anapanda na kama kuna kitu kimetuboa tukwambie. Ulitufanya tujisikie vibaya kuondoka na ilibidi turudi baadae sababu tulikuahidi tunarudi.
 
It was too much for the administration, walisema haiendani na academic values za chuo. Siku wanafunzi walihudhuria kwa wingi mno, mlimani peke yake kuna 30k students. Wengine walizidiwa na starehe na kusababisha usumbufu kwenye residential houses and properties. Uongozi uliona ni vyema kusitisha matumizi. But its one hell of a venue kwa kweli. Tuliweka historia pale.
Pengine walikuwa wanayo point kabisa...kulipeleka pale lazima lilete shida tuu...
Endelea kulipeleka kwenye viwanja vikubwa na vingine vinavyo chukua watu wengi zaidi kulipeleka kwenye viwanja vya vyuo lazima wataanza kuweka masharti yatayo waathiri...
Nina hakika mkijipanga vyema popote watafata na mtaweka historia...
 
Nini kilitokea kwenye kipindi cha siasa za siasa? Nilikipenda kweli kile kipindi.
And naomba nikuambie una customer care nzuri. Last time Nyama Choma Moshi tulikutana na wewe tukiwa tunatoka. Ukatusimamisha like mnaenda wapi mbona mapema au mmeboreka. Tukakuambia tunatoka mara moja tunarudi. Kweli tulikua tumeboreka ila ukatumbia tusubirie Aslay anapanda na kama kuna kitu kimetuboa tukwambie. Ulitufanya tujisikie vibaya kuondoka na ilibidi turudi baadae sababu tulikuahidi tunarudi.

Oh wow! That was you! Nashukuru wangu..kwanza kwa kuja..na pili kwa kuitikia wito. Wateja wetu ni kila kitu kwetu. Thank you for the support.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom