Carrymastory, Afunguliwa Kesi ya Madai ya Shilingi Milioni 600 na Hamisa Mobetto

Carrymastory, Afunguliwa Kesi ya Madai ya Shilingi Milioni 600 na Hamisa Mobetto

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mwandishi wa habari za burudani nchini Tanzania, Carrymastory, ameweka wazi kuwa amefunguliwa kesi ya madai ya shilingi milioni 600 na mwanamitindo na mfanyabiashara mashuhuri, Hamisa Mobetto.

Kesi hiyo imefunguliwa na mwanasheria pamoja na meneja wa Hamisa Mobetto mwezi Septemba 2026.

Madai hayo yanatokana na video iliyochapishwa na Carrymastory mwaka 2023, yenye urefu wa chini ya sekunde 30, iliyomgusa mfanyabiashara huyo.

Mwandishi huyo ameeleza hisia zake kwa uchungu kupitia ukurasa wake wa Instagram, akibainisha kusikitishwa kwake na hatua hiyo baada ya miaka mitatu tangu video hiyo ichapishwe.

Carrymastory ameeleza kuwa ameshirikiana na kumpigania Hamisa kwenye mitandao ya kijamii kwa zaidi ya miaka minane bila malipo yoyote, ikiwemo kusimama naye wakati wa changamoto mbalimbali za kimahusiano na kifamilia.

Amesisitiza kuwa hana ugomvi na kesi hiyo, bali anaumizwa na ukosefu wa shukrani kutoka kwa msanii huyo aliyemtumikia kwa mapenzi kama shabiki wake namba moja.

Tukio hili limeibua mjadala mpana mtandaoni kuhusu uhusiano kati ya wasanii na mashabiki au wanahabari wanaowasapoti katika kiwanda cha burudani.
1789652407286.png

1789652325584.png
 
Back
Top Bottom