Ninaungana na wale wote wanaomtazama JK kama mtu aliyepewa nafasi nyingi za kurekebisha mambo na akaendelea kuboronga...Hili liwe funzo kubwa kwetu watanzania kuwa mtu aliyeingia madarakani kwa RUSHWA, hatakuwa na nguvu ya kukemea rushwa ......na kwamba anashindwa kukemea uozo wa EPA, BOT, na Richmond, hatuna sababu ya kuhisia na kudhania hisia zetu ni za uongo, huyu jamaa naye yumo katika uozo huu na hivyo anajikuta yuko katika kitanzi.
Kwa akili ya utu uzima aliona nao, angeweza kujua ni nini anapaswa kufanya. Ila kwa vile Rushwa hondoa maarifa, na kuondoa utashi, basi amejikuta mvinyo wa Rushwa ya EPA na Richmond na vimada wa majuu unamlewesha na hata kujisahau kuwa na kiongozi wa watu 35 milioni na si kijitabaka cha kina lowasa na chenge na wake zao!
AIBU KWA JK na washauri wake.